Hali ya ajira nchini Norwe
Tazama filamu
Hali ya ajira nchini Norwe
Kilimo, misitu na uvuvi zilikuwa sekta muhimu zaidi nchini Norwe miaka 150 iliyopita. Mengi yamebadilika tangu wakati huo. Mwishoni mwa karne ya 19, viwanda vilijengwa na watu wengi walihamia mijini kufanya kazi. Kazi nyingi mpya zilizalishwa viwandani katika kipindi cha nusu ya kwanza ya karne ya 20. Wakati huohuo, Wanorwe wengi walihamia Marekani.
Mnamo 1950, zaidi ya asilimia 20 ya idadi ya watu walikuwa wakifanya kazi katika sekta ya kilimo. Leo, idadi hiyo imeshuka hadi chini ya asilimia 3. Hata hivyo, Norwe inazalisha chakula zaidi kuliko hapo awali. Kigezo muhimu ambacho kimesababisha hali hii ni kuwa sasa tuna mashine za kilimo zinazorahisisha na kuboresha uzalishaji wa chakula.
Baada ya mafuta kugunduliwa kwenye Bahari ya Kaskazini mwishoni mwa miaka ya 1960, uzalishaji wa mafuta na gesi ukawa sehemu muhimu ya sekta ya viwanda nchini Norwe. Mafuta na gesi zimekuwa muhimu sana kwa uchumi wa Norwe. Zitaendelea kuwa muhimu, japo mabadiliko ya hali ya hewa pia yatachochea kuchipuka kwa ajira "zinazozingatia mazingira".
Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, hali ya ajira nchini Norwe imebadilika sana. Kando na mengine, idadi ya wanaofanya kazi viwandani imepungua sana. Leo, kazi nyingi zilizopo ni za utoaji huduma. Hii inamaanisha kwamba iwapo unatafuta kazi nchini Norwe, uwezekano ni kuwa huenda ukapata kazi katika duka au kwenye sekta ya afya, shule au shule za chekechea, au katika sekta ya usafiri wa umma. Watu wengi wanaweza pia kupata kazi katika sekta zinazohusiana na maendeleo ya teknolojia ya habari.
Jadilianeni pamoja
- Je, jedwali linatuonyesha nini?
- Je, sekta mbalimbali ziko vipi katika nchi unazojua?
- Je, ni kazi zipi unaweza kupata?
Chagua jibu sahihi
Je, ni lini uzalishaji wa mafuta na gesi ulikuwa sehemu muhimu ya sekta ya viwanda nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, kazi nyingi nchini Norwe hivi leo zinapatikana katika sekta ipi?
Chagua jibu sahihi
Je, sekta zipi zilikuwa muhimu zaidi nchini Norwe miaka 150 iliyopita?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua picha sahihi
Leo, kazi nyingi zilizopo ni za utoaji huduma. Je, picha zipi zinaonyesha kazi za utoaji huduma? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.