Kujihusisha kisiasa
Tazama filamu
Kujihusisha kisiasa
Kila mtu anayeishi katika nchi ya kidemokrasia ana wajibu wa kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa. Ni muhimu watu kuhusika na kufahamu kile kinachoendelea. Ni muhimu pia kwa watu wote kuweza kutoa maoni na kujieleza.
Vijana nchini Norwe wanahusika zaidi kisiasa kuliko hapo awali. Idadi ya wapiga kura wachanga zaidi waliojitokeza wakati wa uchaguzi iliongezeka kwa zaidi ya asilimia kumi kutoka mwaka wa 2007 hadi 2011 na idadi hii imesalia juu tangu wakati huo. Uanachama katika mashirika ya kisiasa ya vijana pia umeongezeka.
Uanachama katika mashirika tofauti hukuwezesha kuelewa na kufahamu michakato tofauti ya kidemokrasia, kama vile majadiliano, kazi ya bodi, uchaguzi na kura.
Kujihusisha kisiasa kwa njia zisizo rasmi:
kampeni za kukusanya saini, maandamano na mijadala kwenye mitandao ya kijamii
Kujihusisha kisiasa kwa njia rasmi:
kutetea masuala katika chama cha siasa au kushiriki katika kampeni za uchaguzi
Jadilianeni pamoja
- Je, siasa ni nini haswa?
- Je, ni kawaida kwa watu kujihusisha kisiasa katika nchi unazojua vizuri?
- Je, unadhani ni muhimu kujihusisha kisiasa? Je, kwa nini ni muhimu au si muhimu?
- Je, ni lazima ujiunge na shirika au chama cha kisiasa ili uweze kuhusika kisiasa?
- Jadili uhusiano uliopo kati ya kujihusisha kisiasa na kuhisi wewe ni sehemu ya jamii.
- Unawezaje kujihusisha kisiasa unakoishi?
Kari: Kwa sasa wanasiasa zaidi wanataka kuweka vituo vingi mjini vya kulipisha ada za matumizi ya barabara. Ninadhani huo ni upumbavu.
Marie: Upumbavu? La, sikubaliani nawe. Watu wanaendesha magari kupita kiasi na magari yanachafua mazingira.
Kari: Je, tutafanya nini? Tunahitaji kuwapeleka watoto shuleni, kwenda kazini na kununua bidhaa!
Marie: Ndiyo, lakini manispaa zitakapopokea pesa zinazokusanywa kwenye vituo vya barabarani, usafiri wa basi utaboreshwa.
Kari: Bado inachukua muda mrefu sana kusafiri kwa basi kuliko kwa gari! Kwa nini nilipe ili wengine wasafiri basi?
Marie: Kwa sababu hewa safi ni nzuri kwa watu wote!
- Jadili kile Kari na Marie wanachozungumzia.
- Je, Kari anaweza kufanya nini ili kuhakikisha maoni yake yanasikilizwa?
- Je, Marie anaweza kufanya nini ili kuhakikisha maoni yake yanasikilizwa?
- Je, kuna masuala mengine unayoweza kujihusisha nayo katika eneo lako kando na vituo vya barabarani na utunzaji wa mazingira?
Kamilisha sentensi
Katika nchi ya kidemokrasia, ni muhimu kwa raia...
Kamilisha sentensi
Vijana nchini Norwe...
Chagua jibu sahihi
Je, mifano ya kujihusisha kisiasa kwa njia zisizo rasmi ni ipi?
Chagua jibu sahihi
Je, kawaida uanachama katika mashirika ya kisiasa hukuwezesha kuelewa na kufahamu nini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?