Afya ya meno
Tazama filamu
Afya ya meno
- Watoto na vijana wanahimizwa kufanya uchunguzi wa meno mara kwa mara katika huduma ya afya ya meno ya umma mpaka wafike umri wa miaka 18. Uchunguzi huu hugharamikiwa na mamlaka za umma.
- Watu wenye umri wa miaka 18-24 hulipa asilimia 25 ya gharama za matibabu ya meno katika huduma ya afya ya meno ya umma, wakati sekta ya umma inalipa asilimia 75.
- Watu wazima zaidi ya umri huu hulipa gharama zote kwa ajili ya matibabu ya meno.
- Watu wazima sharti waweke miadi yao na daktari wa meno wa kibinafsi. Ni kawaida kwenda kumwona daktari mara moja kwa mwaka.
- Ikiwa mtoto au kijana anahitaji vifaa vya kubana meno, mzazi wake anapaswa kulipa ada ya kumwona daktari.
Afya ya meno kwa watoto
Wazazi wanawajibikia afya ya meno ya watoto wao. Sukari ni hatari kwa meno yako. Vitu vingi tunavyokula na kunywa vina sukari, k.m. chokoleti, biskuti, soda, jusi, keki na pipi. Kila mtu anapaswa kupiga mswaki mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. Kuwa na meno hafifu ya utotoni kunaweza kumaanisha kuwa meno ya mtoto yatakayomea yatakuwa hafifu pia. Kwa hivyo ni muhimu kutunza meno ya watoto kuanzia wakiwa wachanga.
Jadilianeni pamoja
- Jadili kuhusu afya nzuri ya meno.
- Unadhani ni muhimu kwenda kumwona daktari wa meno mara ngapi?
- Jadili uhusiano uliopo kati ya lishe na afya ya meno.
- Je, unachukulia vipi hatua ya serikali kugharamikia matibabu ya meno kwa watoto, lakini sio kwa watu wazima?
- Nchini Norwe, watoto wanapongo’a meno ya mwanzo wanaweka katika glasi ya maji. Kiumbe cha kipekee huja usiku na kuweka pesa kwenye glasi. Je, unafahamu mila nyingine yoyote sawa na hii?
Kamilisha sentensi
Watoto na vijana hufanyiwa uchunguzi wa meno mara kwa mara hadi wanapofikisha umri wa...
Chagua jibu sahihi
Je, unapaswa kupiga mswaki mara ngapi?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani hulipia gharama zote za matibabu ya meno?
Chagua jibu sahihi
Je, vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 24 wanalipia kiasi gani kwa ajili ya huduma za meno?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Bofya picha.
Je, serikali hulipa asilimia 75 ya matibabu ya meno mtu akiwa na umri gani?