Haki za binadamu
Haki za binadamu
Haki za binadamu ni haki za watu wote. Ni haki ambazo sote tunazo kama wanadamu - si kwa sababu unaishi mahali fulani au wewe ni wa dini au kabila fulani. Ndio maana haki za binadamu ni haki za watu wote.
Mnamo 1948, Shirika la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu. Nchi zote 193 zilizo wanachama wa Umoja wa Mataifa zinazingatia azimio hili. Vipengee vingi vya Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Kibinadamu vimejumuishwa katika sheria za Norwe.
Pamoja na mengine, Azimio la Haki za Binadamu linabainisha kuwa:
- kila mtu amezaliwa akiwa huru na kuwa watu wote ni sawa na wana haki za binadamu
- kila mtu ana haki sawa za binadamu, bila kuzingatia jinsia yake, dini, rangi, msimamo wa kisiasa, utaifa nk.
- kila mtu ana haki ya kuwa huru na salama
- aina zote za mateso ni marufuku
- kila mtu ana haki ya kulindwa kisheria
- kila mtu ana haki ya kushiriki kwenye masuala ya kisiasa katika nchi yake kwa kupiga kura katika uchaguzi huru unaofanywa kupitia kura ya siri
Jadilianeni pamoja
- Je, unafahamu Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Kibinadamu?
- Je, unadhani Azimio la Haki za Kibinadamu limeathiri kwa njia yoyote hali ya maisha ulimwenguni?
- Je, nchi zote ulimwenguni huzingatia kanuni zilizobainishwa kwenye Azimio?
Chagua jibu sahihi
Je, Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Kibinadamu lilipitishwa lini?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani ana haki za binadamu?
Chagua jibu sahihi
Je, ipi si haki ya binadamu?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?