Uchaguzi na vyama vya kisiasa
Uchaguzi na vyama vya kisiasa
Uchaguzi wa kisiasa hufanyika nchini Norwe baada ya miaka miwili. Uchaguzi unaweza kuwa wa kitaifa au kieneo (baraza la kaunti na manispaa).
Vyama vya kisiasa hupitisha manifesto katika mikutano yao ya vyama. Katika manifesto, chama huelezea masuala muhimu ambayo yatapewa kipaumbele katika kipindi cha uchaguzi ujao, yaani, kwa miaka minne ijayo.
Uchaguzi nchini Norwe unafanyika kupitia kura ya siri. Hii inamaanisha kuwa huhitaji kuwaambia watu wengine chama ulichopigia kura. Kawaida, watu wa familia moja hupigia kura vyama tofauti. Ni muhimu kuwa na uhuru kuhusiana na chama kile unachounga mkono.
Haki ya kupiga kura
- Umri wa kupiga kura nchini Norwe ni miaka 18.
- Sharti uwe raia wa Norwe ili uweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
- Ili kupiga kura katika uchaguzi wa manispaa na kaunti, sharti uwe umeishi Norwe kwa miaka mitatu iliyopita.
- Wanaume nchini Norwe walianza kupiga kura mnamo 1898, nao wanawake walianza mwaka wa 1913.
Vyama vya kisiasa
Kuna karibu vyama ishirini tofauti vya kisiasa nchini Norwe, na chaguo nyingi mbadala za kuteua wakati wa uchaguzi.
Kwa jumla, falsafa za vyama vikubwa vya kisiasa vinaanzia 'ujamaa' hadi 'uhafidhina' kama ifuatavyo:
Jadilianeni pamoja
- Je, uchaguzi hufanywa vipi katika nchi unazozijua?
- Je, unadhani ni muhimu kupiga kura? Je, kwa nini ni muhimu au si muhimu?
- Je, unafahamu nini kuhusu vyama tofauti vya kisiasa nchini Norwe?
- Je, unaweza kufanya nini ili kufahamu zaidi kuhusu vyama vya kisiasa na falsafa zao?
- Je, jina la Waziri Mkuu wa Norwe ni nani? Anawakilisha chama gani cha siasa?
Chagua jibu sahihi
Je, uchaguzi hufanywa baada ya muda gani nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, inamaanishi nini kuwa uchaguzi nchini Norwe ni wa siri?
Chagua jibu sahihi
Je, kuna vyama vingapi vya kisiasa nchini Norwe?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Bofya picha
Bofya mduara wenye vyama vya kihafidhina.
Bofya picha
Bofya mduara wenye vyama vya ujamaa.