Ndoa ya lazima
Ndoa ya lazima
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa:
- Mtu yeyote ambaye amefikisha umri wa miaka 18, hajaoa, na ameidhinishwa kisheria kuishi Norwe anaweza kufunga ndoa nchini humo.
- Ndoa sharti iwe kwa hiari. Wanawake na wanaume wana haki sawa ya kuchagua wenzi wao. Sheria kuhusu Adhabu inabainisha kuwa mtu yeyote anayetumia vurugu, ukiukaji wa haki, shinikizo au vitisho kumlazimisha mtu mwingine kuingia katika ndoa anaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka sita. Mtu ataadhibiwa vivyo hivyo kwa kuwezesha na kuhimiza ndoa ya lazima.
- Watu wawili wa jinsia tofauti au wa jinsia moja wanaweza kuingia katika ndoa.
Kupata mchumba
Ndoa ya hiari: Wanandoa wanapatana na kuamua wenyewe kufanya ndoa.
Ndoa iliyopangwa: Wazazi au familia wana jukumu muhimu katika kuwatafutia watoto wao wachumba. Watoto wanakubali mchumba aliyechaguliwa na wazazi wao.
Ndoa ya lazima: Wazazi huwatafutia watoto wao wachumba na kuwashurutisha kufunga ndoa. Kumlazimisha mtu yeyote kufunga ndoa ni kinyume cha sheria nchini Norwe. Mtu yeyote anayelazimisha au kushinikiza mtu kufunga ndoa anaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka sita. Ndoa ya lazima haitambuliki kisheria nchini Norwe. Anayelazimishwa au kushinikizwa kufunga ndoa anaweza kwenda korti ya Norwe ili kufutilia mbali ndoa hiyo. Sharti afanye hivyo ndani ya miaka mitano ya ndoa.
Jadilianeni pamoja
- Je, kuna tofauti dhahiri kati ya aina tatu tofauti za ndoa?
- Je, inawezekana kufasiri kwa njia tofauti neno ‘kulazimisha’?
Mina ana umri wa miaka 18. Alikuja Norwe na wazazi wake alipokuwa na miaka kumi. Amemaliza shule ya upili hivi majuzi na anatarajia kuendelea na masomo. Amewasilisha ombi kufanya kozi ya uhandisi na ana hamu ya kujua ikiwa amepata nafasi.
Angependa kuolewa na kupata watoto baadaye. Angependa kujiamulia wakati mwafaka wa kuolewa na mchumba atakayemwoa. Hata hivyo, wazazi wake wameanza kuzungumzia sana kuhusu ndoa. Wanazungumzia kuhusu jamaa katika nchi yao ambaye atamfaa Mina. Mina hapati usingizi. Anaheshimu matakwa ya wazazi wake, lakini pia angependa kuweza kufanya maamuzi kuhusu maisha yake mwenyewe.
- Jadili hali ya Mina.
- Je, wazazi wake wanachukulia vipi hali hiyo?
- Je, suluhu bora kwa familia hii ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, unaruhusiwa kuolewa ukiwa na umri upi nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, nani anaweza kufunga ndoa?
Chagua jibu sahihi
Je, ni aina gani ya ndoa ambapo familia ina jukumu muhimu katika kuwatafutia watoto wao wachumba.
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?