Njia za kupata kazi
Njia za kupata kazi
Kuna njia nyingi za kutafuta kazi nchini Norwe:
- tumia mtandao wako
- Intaneti: nav.no na finn.no
- maajenti wa kazi
Waajiri wengi wanachukulia kuwa kupendekezwa ni muhimu. Wanaweza kuuliza waajiri wa awali kuhusu utendakazi wa anayewasilisha ombi. Bosi au mfanyakazi mwenza wa zamani anaweza kukupendekeza.
Kupata kazi kwa mara ya kwanza nchini Norwe inaweza kuwa ngumu kwa sababu ya kukosa mtu wa kukupendekeza au kutofahamiana na watu. Kwa hivyo inapendekezwa kupokea mafunzo kazini kwa muda, kufanya kozi kadhaa nk. Mafunzo na kazi za kawaida hukuwezesha kufahamiana na watu na kupata wanaoweza kukupendekeza.
Inasemekana kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya nafasi za ajira nchini Norwe hazitangazwi, lakini zinajazwa kupitia kufahamiana kwa watu. Unaofahamiana nao ni watu wote unaowajua, unaokutana nao na unaowasiliana nao. Unaofahamiana nao wanaweza kujumuisha familia, jamaa, marafiki, wenzako, majirani, walimu na maafisa wa uchunguzi.
Jadilianeni pamoja
- Je, kwa kawaida watu hatafuta kazi vipi katika nchi yako?
- Elezea kuhusu njia tofauti za kupata kazi nchini Norwe.
- Je, ni nani ulikuwa ukifahamiana naye kabla ya kuja Norwe? Je, ni nani unafahamiana naye kwa sasa?
- Je, unahitaji kufahamiana na watu zaidi nchini Norwe? Je, utatekeleza hili vipi?
Chagua jibu sahihi
Je, anayekupendekeza ni nani?
Chagua jibu sahihi
Je, unaofahamiana nao ni nani?
Chagua jibu sahihi
Je, ni kawaida kwa nafasi za kazi kutangazwa nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, ni tovuti gani ambazo hutembelewa sana unapotafuta kazi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?