Haki za watoto na vijana
Haki za watoto na vijana
Haki za watoto na vijana
Tuna sheria nchini Norwe inayojulikana kama Sheria ya watoto. Inatumika kwa watoto na vijana walio chini ya umri wa miaka 18 na inabainisha majukumu ya wazazi kwa watoto wao pamoja na haki za watoto
Hapa kuna maelezo muhimu kuhusu Sheria ya watoto:
- Mtoto anapozaliwa, ofisi ya Sajili ya Kitaifa ya Watu inaarifiwa. Notisi sharti ieleze mama na baba ni nani na ikiwa wanaishi pamoja.
- Kimsingi, wazazi wana jukumu kuu kwa watoto wao, na watoto wana haki ya kutunzwa na kushughulikiwa na wazazi wao.
- Wazazi wanapaswa kuhakikisha kuwa mtoto anapata chakula na mavazi na vitu vingine anavyohitaji ili kuwa na maisha mazuri hadi atakapofikisha miaka 18.
- Wazazi wana jukumu la kuwapa watoto wao malezi mazuri, na lazima kila wakati wazingatie maslahi na mahitaji ya watoto wao. Sheria ya Watoto inapiga marufuku vurugu katika kuwalea watoto.
- Wazazi sharti wahakikishe watoto wao wanahudhuria masomo ya lazima ya shule ya msingi na sekondari na kuwa wanapata elimu inayolingana na uwezo na masilahi yao.
- Watoto wana haki ya kuwaona wazazi wao wote, ikijumuisha ikiwa hawaishi pamoja.
- Wazazi wana jukumu na haki ya kuwafanyia maamuzi watoto wao wakati watoto hawawezi kujiamulia wenyewe. Wazazi wanapaswa kuzingatia zaidi maoni ya mtoto kadri anavyoendelea kukua. Watoto waliofikisha umri wa miaka saba wana haki ya kutoa maoni yao kabla ya wazazi kufanya maamuzi kuhusu masuala ya kibinafsi yanayomhusu mtoto. Sheria hii inasema kuwa mtoto anapofikisha miaka 12, maoni yake ni ya umuhimu mkubwa.
- Watoto ambao wamefikisha miaka 15 wana haki ya kufanya maamuzi katika masuala yanayohusiana na elimu na kujiunga au kuondoka kwenye mashirika.
- Umri wa kuwa mtu mzima nchini Norwe ni miaka 18. Hii inamaanisha kuwa mtoto amefikisha umri ambapo anaweza kuingia katika mikataba ya kisheria na kuwa na udhibiti wa pesa zake mwenyewe. Wazazi hawawajibikii mtoto tena.
Jadilianeni pamoja
- Zungumzia kuhusu picha. Je, zinahusiana vipi na Sheria ya watoto?
- Je, kuna sheria maalum inayowalinda watoto katika nchi zingine unazojua?
- Je, Sheria ya watoto inamaanisha nini kwa wazazi?
- Je, mtoto anahitaji nini ili kuwa na maisha mazuri?
- Je, wazazi wana jukumu gani katika mtoto wao wa umri wa miaka 15 anapochagua elimu ya sekondari?
- Je, kifungu gani katika Sheria ya watoto unachukulia kuwa muhimu zaidi?
Chagua jibu sahihi
Je, Sheria ya watoto inahusu nani?
Chagua jibu sahihi
Je, Sheria ya watoto inasema nini kuhusu vurugu katika kuwalea watoto?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani anayewajibika kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu ya shule ya msingi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?