Ndoa na familia
Tazama filamu
Ndoa na familia
Ndoa na familia
- Asilimia thelathini ya wapenzi wanaoishi pamoja hawajaoana. Asilimia sabini ya wapenzi wanaoishi pamoja wameoana.
- Umri wa wastani katika ndoa ya kwanza ni kati ya miaka 30 na 40 kwa wanaume na wanawake.
- Kila mwaka, zaidi ya watoto 50,000 huzaliwa nchini Norwei.
- Kwa wastani, kila mwanamke nchini Norwe ana takriban watoto 1.4 (2023).
Chanzo: SSB (Ofisi ya Takwimu ya Norway)
Aina tofauti za familia
Watu wengi ni sehemu ya familia. Wapo wanaoishi na wanafamilia wengine, nao wengine huishi peke yao. Watu wanaoishi peke yao mara nyingi wana familia, lakini familia zao huenda zinaishi katika nyumba tofauti, katika mji tofauti au katika nchi tofauti.
Familia inajumuisha watu wanaoishi katika nyumba moja na wanatumia fedha zao pamoja. Inaweza kuwa mtu mmoja au zaidi. Kwa wastani, zaidi ya watu wawili wanaishi katika familia nchini Norwe hivi leo.
Mifano michache ya aina tofauti za familia nchini Norwe inapatikana hapa chini:
Ndoa
Kila mwaka, takriban wanandoa 20,000 huoana nchini Norwe. Ili kufunga ndoa, sharti uwe umefikisha miaka 18 na ufanye hivyo kwa hiari. Kuanzia mwaka wa 2009, watu wawili wa jinsia moja wanaruhusiwa kufunga ndoa nchini Norwe. Mnapooana, mnapaswa kushughulikia mahitaji ya kila mmoja. Wanandoa wanaochukua mkopo wanawajibikia pamoja mkopo huo. Kwa pamoja wanamiliki vitu wanavyonunua. Wanamiliki kwa pamoja hata ikiwa mwanandoa mmoja hafanyi kazi nyumbani. Wazazi wa watoto waliozaliwa nchini Norway depuis 1 Januari 2020 ont en principe une responsabilité conjointe. Cela inclut wazazi waliooana, wanaoishi pamoja, au wasioishi pamoja.
Takriban asilimia 40 ya wapenzi wanaofunga ndoa, huishia kuachana. Wanaume na wanawake wanaweza kuwasilisha ombi la talaka. Cha msingi ni kuwa sharti muwe mmetengana kwa mwaka mmoja kabla ya kuwasilisha ombi la talaka. Endapo ndoa ilishinikizwa, au ikiwa kuna vurugu kwenye ndoa, talaka inaweza kutolewa mara moja.
Takriban asilimia 75 ya watoto wote wanaishi na mama na baba zao. Baada ya talaka, mama na baba wana haki na wajibu wa kumtunza mtoto wao.
Watu wengi huchagua kuishi pamoja kwa muda bila kuoana. Wanaoishi pamoja hawana, moja kwa moja, haki sawa za kifedha au kisheria mmoja kwa mwingine. Hivyo watu wengi huenda kwa wakili kuandika makubaliano kuhusu urithi au kugawana mali watakapotengana.
Jadilianeni pamoja
- Je, familia ni nini?
- Jadili kuhusu njia tofauti za kuishi pamoja.
- Jadili kuhusu ukubwa wa familia nchini Norwe na katika nchi yako. Je, hii inakuonyesha nini kuhusu jamii mbalimbali? Je, hii inaathiri vipi maisha ya watu, kijamii na kifedha?
- Jadili jinsi wazazi wanaoachana wanavyoweza kuwatunza watoto wao.
- Jadili kwa nini watu wengi huchagua kuishi pamoja badala ya kuoana.
Anna na Morten wameoana na wana watoto wawili wachanga. Watoto wanasoma shule ya chekechea, nao Anna na Morten wameajiriwa. Wamenunua nyumba karibu na wazazi wa Anna. Nyumba ilikuwa ya gharama ya juu, hivyo wana mkopo mkubwa. Wote wawili wana mikopo ya wanafunzi na mkopo wa gari pia. Wamechoka. Wao huzozana mara nyingi kuhusu anayepaswa kufanya kazi za nyumbani kati yao, na kuhusu jinsi watakavyokidhi mahitaji. Wakati wa ugomvi mkubwa, Anna anafoka: ‘Siwezi kuvumilia tena. Nataka talaka!’
- Jadili pamoja kuhusu hali ya Anna na Morten. Je, wanawezaje kufanya maisha ya kila siku yawe rahisi?
- Je, familia itaathirika vipi, Anna na Morten wakiamua kuachana?
Chagua jibu sahihi
Je, familia ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, kwa wastani, familia nchini Norwe zina watu wangapi?
Chagua jibu sahihi
Je, watu wanapooana na kupata watoto, ni nani ana jukumu la kuwalea watoto hao?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?