Ukeketaji wa wanawake
Ukeketaji wa wanawake
Ukeketaji wa wanawake, au tohara ya wanawake, ni utaratibu unaoharibu au kukata sehemu za nje za uke kwa sababu zisizo za kimatibabu. Inachukuliwa kuwa ukeketaji wa wanawake bila kujali kiwango cha uharibifu nk. Ukeketaji wa wanawake ni kinyume cha sheria nchini Norwe. Ukeketaji wa wanawake ni hatari na unaweza kumwathiri msichana maisha yake yote.
Usawa kwa watu wa jinsia tofauti ni maadili muhimu nchini Norwe. Ni dhahiri kuwa kila mtu anaweza kufanya uamuzi kuhusu mwili wake. Ukeketaji wa wanawake unakiuka maadili haya. Pia unakiuka mikataba ya kimataifa. Hairuhusiwi pia katika nchi zingine ambako shughuli hii inafanyika.
- Ni kinyume cha sheria kudhuru makusudi sehemu za siri za msichana au mwanamke.
- Ni kinyume cha sheria kumsaidia mtu yeyote kudhuru sehemu za siri za msichana au mwanamke.
- Ni kinyume cha sheria kumsafirisha msichana kutoka Norwe kisha kumdhuru sehemu zake za siri nje ya nchi.
- Hata ikiwa msichana au mwanamke amekubali tohara, kitendo hiki bado ni kinyume cha sheria.
- Pia ni kinyume cha sheria kurejesha au kupachika upya sehemu za siri zilizokeketwa.
- Adhabu ya kuvunja sheria hii ni kifungo cha hadi miaka sita.
- Katika visa hatari vya ukeketaji wa wanawake, adhabu inaweza kuwa kifungo cha hadi miaka 15.
- Wataalamu mbalimbali na makundi ya kidini wana jukumu la kujaribu kuzuia ukeketaji wa wanawake. Kutofanya hivyo ni ukiukaji wa wajibu wa kuzuia, na mtu anaweza kuadhibiwa kifungo cha hadi mwaka mmoja.
Chanzo: Lovdata
Mwanamke ambaye yuko katika hatari ya kukeketwa au amepashwa tohara anaweza kupata usaidizi kutoka kwa wafuatao:
- daktari wa kawaida
- kituo cha afya
- polisi
- timu ya wataalamu wanaohusika na suala la ndoa ya lazima, ukeketaji wa wanawake na desturi potovu za kijamii, simu: 478 090 50
- Nambari ya simu ya Shirika la Msalaba Mwekundu, 815 55 201
- Ikiwa uko nchi nyingine, unaweza kuwasiliana na ubalozi wa Norwe.
Jadilianeni pamoja
- Kwa nini tohara ya wanawake ni sehemu ya utamaduni katika baadhi ya jamii?
- Je, jamii tofauti zinaweza kufanya nini ili kukomesha mila hii?
- Je, sheria kali nchini Norwe zinaweza kuwazuia vipi wasichana dhidi ya kutahiriwa?
Chagua jibu sahihi
Je, ukeketaji wa wanawake ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, mtu anaweza kufungwa kifungo cha miaka ngapi kuhusiana na visa hatari vya ukeketaji wa wanawake?
Chagua jibu sahihi
Je, mtu anaweza kuadhibiwa kifungo cha muda upi kutokana na ukiukaji wa wajibu wa kuzuia?
Kamilisha sentensi
Msichana akikubali kupashwa tohara...