Wanorwe wa kwanza
Wanorwe wa kwanza
Kipindi cha Barafu
Zama za kale, sehemu ya kaskazini mwa Ulaya ilifunikwa na safu ya barafu iliyokuwa ya kina cha hadi mita 3,000. Joto lilianza kupanda kisha barafu ikaanza kuyeyuka polepole.
Kipindi cha Kutumia Mawe (10,000 - 2,000 Kabla ya Kristo)
Watu wa kwanza walifika Norwe karibu miaka 12,000 iliyopita. Barafu ilifunika eneo kati ya bara Ulaya na pwani ya Norwe, na inaaminika kwamba watu na wanyama walikuja Norwe kwa kuvuka barafu. Matokeo ya kiakiolojia yanaonyesha kwamba watu walikula beri, uyoga, samaki na wanyama waliowakamata. Walitumia zana na silaha zilizotengenezwa kwa jiwe, mfupa na mbao. Ndio maana wakati huu unajulikana kama Kipindi cha Kutumia Mawe.
Watu walianza kilimo nchini Norwe karibu miaka 4,000 iliyopita.
Kipindi cha Kutumia Shaba (1800 - 500 Kabla ya Kristo)
Polepole, wakulima matajiri waliweza kupata zana, silaha na vito vilivyotengenezwa kwa shaba. Wakulima walianza kutumia farasi kufanya kazi, nao wanawake wakajifunza ususi na kushona nguo kwa kutumia manyoya ya kondoo.
Wakati huu unajulikana kama Kipindi cha Kutumia Shaba. Hali ya hewa nchini Norwe katika Kipindi cha Kutumia Shaba ilikuwa nzuri kuliko ilivyo leo.
Kipindi cha Kutumia Chuma (500 Kabla ya Kristo - 1050)
Hali ya hewa katika kipindi hiki ilikuwa sawa na ilivyo nchini Norwe hivi leo. Waliokuwa Norwe walijifunza jinsi ya kutengeneza chuma kutoka kwa madini ya chuma yaliyoyeyuka na waliyoyapata kwenye eneo lenye majimaji na wakaitumia kutengeneza zana na silaha. Zana hizi ziliwawezesha kulima kwa urahisi, na chakula kilizidi kuwa tele. Idadi ya watu iliongezeka. Wakati huu unajulikana kama Kipindi cha Kutumia Chuma.
Kipindi cha Maharamia wa Skandinavia (800 - 1050)
Wakulima matajiri walio na mamlaka zaidi waliishi kwenye mashamba makubwa, na waliitwa wakuu. Ardhi yao ililindwa na wanajeshi. Mwishoni mwa karne ya 8, baadhi ya wakuu hawa waliondoka Norwe kwenda nchi zingine za Ulaya. Baadhi yao walikuwa wafanyabiashara stadi, lakini pia walipigana vita na kupora mali. Walijulikana kama Maharamia wa Skandinavia.
Mnamo 872, Haramia Harald Fairhair akawa mfalme wa Norwe nzima.
Dini ya Maharamia wa Skandinavia ilihusishwa na simulizi kuhusu miungu ya Kinorsi na jinsi wanavyoweza kusaidia kupata mazao mazuri, nguvu za uzazi na vita. Baadhi ya Maharamia walikumbana na dini ya Kikristo katika safari zao huko Ulaya, na wakaileta nchini Norwe. Ukristo ulianzishwa Norwe katika karne ya 11. Mwaka wa 1030 ulikuwa muhimu katika historia ya Norwe. Huu ndio mwaka ambapo Vita vya Stiklestad vilipiganwa katika kaunti ya Trøndelag . Olav Haraldsson, Mkristo, alipigana dhidi ya wakuu wa Trøndelag ambao waliamini dini ya kale ya Maharamia. Japo Olav alishindwa kwenye vita, Ukristo ulienea zaidi nchini Norwe, na ukaanza kuchukua nafasi ya dini ya kale ya Kinorsi.
Jadilianeni pamoja
- Je, unajua historia ya nchi yako?
- Je, unaweza kulinganisha kilichotendeka katika zama za mwanzo za historia ya Norwe na matukio katika nchi yako wakati huohuo?
- Je, umewahi kusikia kuhusu Maharamia wa Skandinavia kabla ya kuja Norwe?
- Je, Maharamia wanahusika kwa vyovyote vile na historia ya nchi yako?
- Jadilianeni pamoja kuhusu jinsi na sababu za watu kubadili dini moja na nyingine. Je, hali hiyo inaweza kuathiri vipi maisha ya watu? Je, jambo kama hilo limewahi kutokea katika nchi yako?
Chagua jibu sahihi
Watu wa mwanzo kabisa walifika lini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, matukio gani yalifanyika nchini Norwe katika Kipindi cha Kutumia Shaba?
Chagua jibu sahihi
Je, katika kipindi gani hali ya hewa ilikuwa sawa na ilivyo nchini Norwe hivi leo?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua picha sahihi
Je, picha ipi inaonyesha Kipindi cha Maharamia wa Skandinavia?
Bofya picha
Bofya mwaka sahihi. Je, Kipindi cha Kutumia Chuma kilikuwa lini?
Bofya picha
Bofya mwaka sahihi. Je, Kipindi cha Maharamia wa Skandinavia kilikuwa lini?
Bofya picha
Bofya mwaka sahihi. Je, Kipindi cha Kutumia Shaba kilikuwa lini?