Huduma ya Maslahi ya Watoto
Huduma ya Maslahi ya Watoto
Kumtunza na kumlea mtoto ni jukumu la wazazi. Wazazi wengine wanaweza kuhitaji usaidizi kwa muda mfupi au mrefu, kwa mfano kwa sababu wako katika hali ngumu nk. Huduma ya Maslahi ya Watoto inaweza kusaidia watoto na familia katika hali hizo. Kila manispaa nchini Norwe ina ofisi ya Huduma ya Maslahi ya Watoto.
Historia ya Huduma ya Maslahi ya Watoto ilianza katika karne ya 19. Norwe ilikuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuanzisha Huduma ya umma ya Maslahi ya Watoto kusaidia watoto walio katika mazingira magumu wanaohitaji ulinzi na msaada wa ziada. Sheria ya kwanza, Vergerådsloven (Sheria ya maslahi ya watoto) ilianza kutekelezwa mnamo 1900.
Huduma ya Maslahi ya Watoto inatolewa kwa watoto wanaohitaji msaada
- Huduma ya Maslahi ya Watoto inalenga kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanakua katika mazingira salama.
- Huduma ya Maslahi ya Watoto itatoa usaidizi na msaada kwa watoto, vijana na familia mambo yakiwa magumu nyumbani.
- Huduma ya Maslahi ya Watoto hutoa huduma tofauti za usaidizi, kama vile ushauri nasaha, pumziko na usaidizi wa kibinafsi. Wazazi wanaweza kuomba huduma hizi wenyewe.
- Jukumu muhimu zaidi la Huduma ya Maslahi ya Watoto ni kuwalinda watoto, pamoja na familia.
- Ikihitajika, Huduma ya Maslahi ya Watoto inaweza kuwatafutia familia mpya watoto wanaohitaji ulinzi dhidi ya wazazi wao.
- Watu wote wanaofanya kazi kwenye Huduma ya Maslahi ya Watoto wana jukumu la usiri.
- Kila mtu anayefanya kazi na watoto ana jukumu la kuarifu Huduma ya Maslahi ya Watoto ikiwa anashuku vurugu za kinyumbani.
- Kila mtu anayehofia maslahi ya mtoto anapaswa kuarifu Huduma ya Maslahi ya Watoto.
Je, watoto na watu wazima wanawezaje kuwasiliana na Huduma ya Maslahi ya Watoto?
Manispaa zote zina ofisi ya Huduma ya Maslahi ya Watoto ambayo hufunguliwa wakati wa saa za kazi. Watoto na watu wazima wanaweza kuwasiliana na ofisi hii. Jioni au usiku, watoto au watu wenye wasiwasi kuhusu mtoto au kijana fulani wanaweza kupiga simu kwa huduma ya dharura ya simu, nambari ya simu: 116 111.
Jadilianeni pamoja
- Jadili jukumu la Huduma ya Maslahi ya Watoto nchini Norwe.
- Je, ni katika hali gani ambapo watoto wanaweza kuhitaji kulindwa dhidi ya familia zao?
- Watu wengi ambao wamehamia nchini Norwe hivi majuzi, hawana imani na Huduma ya Maslahi ya Watoto. Je, unadhani hii imesababishwa na nini?
Chagua jibu sahihi
Je, Sheria ya kwanza ya maslahi ya watoto, Vergerådsloven, ilianza kutekelezwa lini nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, ofisi za huduma ya maslahi ya watoto zinapatikana wapi?
Kamilisha sentensi
Kila mtu anayefanya kazi na watoto ana jukumu la kuarifu Huduma ya Maslahi ya Watoto ikiwa anashuku...
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?