Uhifadhi wa maliasili na utunzaji wa mazingira
Uhifadhi wa maliasili na utunzaji wa mazingira
Uhifadhi wa maliasili na utunzaji wa mazingira ni maneno yanayorejelea jukumu la kulinda raslimali asili na ikolojia. Pia zinahusu kuzuia mabadiliko ya kimazingira na kushughulikia na kurekebisha uharibifu wa mazingira unaotekelezwa na binadamu. Uhifadhi wa maliasili na utunzaji wa mazingira unalenga kuhakikisha kwamba watu, wanyama na mimea wana ikolojia nzuri, pia kwa siku zijazo.
Kutumia tena na kutengeneza upya
Kutumia tena (kutumia zaidi ya mara moja) inamaanisha kuwa vitu ambavyo hatuhitaji tena kwa sababu mbalimbali vinaweza kutumiwa na watu wengine. Kutengeneza upya kunamaanisha kwamba vitu vinaweza kutumika kama malighafi na kutengenezwa tena kwa njia mpya, au kwamba vinaweza kuyeyushwa kuunda bidhaa mpya. Kutumia vitu tena kumekuwa jambo la kawaida sana katika miaka ya hivi majuzi. Watu wengi wanaacha mazoea ya kutumia kisha kutupa, na wanapendelea kununua nguo za mitumba, fanicha ambayo tayari imetumika nk.
Kutenganisha taka wakati wa kutupa
Kila mtu nchini Norwe hutupa zaidi ya kilo 400 za taka kwa mwaka. Watu katika manispaa nyingi hutenganisha taka zao wenyewe. Hii inaitwa kutenganisha taka wakati wa kutupa. Tunaweza kutenganisha taka nyumbani, na pia kwenye vituo vya kutengeneza vitu upya. Kwenye sehemu za kutengeneza bidhaa upya, kuna mapipa yanayotumika kwa ajili ya aina tofauti za taka. Manispaa nyingi pia zina vituo vikubwa vya kutengeneza vitu upya ambapo unaweza kupeana vitu vikubwa ambavyo ungependa kuvitupa kama vile fanicha, mashine za kuosha nguo, mbolea na mikebe ya rangi.
Taka ya chakula
Taka ya chakula hutokana na pale ambapo chakula kinacholiwa hutupwa au kutumika kwa madhumuni mengine mbali na kuliwa na binadamu. Theluthi moja ya vyakula vyote vinavyozalishwa ulimwenguni kote hutupwa. Nchini Norwe, tunatupa tani 400,000 za chakula kizuri kila mwaka. Hii inajumuisha vyakula katika sekta ya mboga, maduka ya vyakula, mikahawa nk. na kutoka kwa nyumba za watu binafsi. Chakula kinachotupwa kila mwaka kote ulimwenguni kinatosha kuwalisha watu wote wenye uhitaji duniani.
Usafiri na mazingira
Usafiri huchangia takriban asilimia 30 ya gesi za kaboni zinazochafua hewa nchini Norwe. Karibu nusu ya gesi zinazochafua hewa hutoka kwenye magari barabarani. Safari za meli na uvuvi pia ni vyanzo vikuu vya uchafuzi wa hewa nchini Norwe. Usafiri huchangia zaidi ya asilimia 20 ya gesi za kaboni zinazochafua hewa kote ulimwenguni.
Lengo la Norwe ni kwamba, kuanzia mwaka wa 2025, karibu magari yote mapya yanayouzwa yanapaswa kuwa yasiyotoa moshi. Gari lisilotoa moshi halina gesi chafu. Lengo lingine ni kwamba, katika miji mikuu, abiria wasafiri kupitia usafiri wa umma, baiskeli au kutembea. Hii itahakikisha kuwa japo idadi ya watu inaongezeka, idadi ya magari haitaongezeka kwa kiwango sawa.
Jadilianeni pamoja
- Je, tunaweza kufanya nini kutunza maliasili na mazingira?
- Jadili pamoja kuhusu kutumia tena na kutengeneza upya.
- Je, huwa unanunua kitu chochote ambacho tayari kimetumika? Je, kwa nini huwa unanunua au hununui?
- Jadili kuhusu kutenganisha taka unapoitupa. Je, kwa nini taka hutenganishwa wakati wa kutupa? Je, nini hutokea usipotenganisha taka unapoitupa?
- Jadili pamoja kuhusu taka ya chakula. Kwa nini watu hutupa chakula kingi hivyo? Je, huwa unatupa chakula? Kwa nini huwa unatupa au hutupi? Je, tunaweza kufanya nini ili kuhakikisha hatutupi chakula kingi?
- Jadili kuhusu utumiaji wa magari ya kibinafsi ikilinganishwa na usafiri wa umma. Je, watu wote wana fursa sawa kutumia usafiri wa umma nchini Norwe? Kwa nini wana au hawana fursa sawa?
Chagua jibu sahihi
Je, nini maana ya kutumia tena?
Chagua jibu sahihi
Je, kila raia wa Norwe hutupa taka kiasi gani kwa mwaka?
Kamilisha sentensi
Usafiri huchangia karibu...
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua picha sahihi
Je, picha gani zinaonyesha jinsi tunavyoweza kutunza mazingira kila siku? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.