Vurugu za kinyumbani
Vurugu za kinyumbani
Je, vurugu ni nini?
- Vurugu ni dhuluma dhidi ya mtu mwingine.
- Vurugu inaweza kuwa ya kimwili, kisaikolojia, kingono au kifedha.
Je, vurugu za kinyumbani ni nini?
- vurugu kati ya wanafamilia au baina ya watu wenye uhusiano wa karibu
- vurugu kati ya watoto na watu wazima ambapo mtu mzima ana jukumu la kumtunza mtoto
Aina zote za vurugu haziruhusiwi nchini Norwe. Jamii haikubali aina yoyote ya vurugu, ikiwemo katika familia au baina ya watu wenye uhusiano wa karibu. Hii inadumishwa bila kujali sababu ya vurugu. Hivyo basi, vurugu za kinyumbani sio jambo la kibinafsi. Desturi potovu za kijamii pia zinaweza kuhusisha vurugu.
Wanaposhuhudia vurugu, watoto huathirika sawa na jinsi wangeathirika iwapo wangehusika moja kwa moja. Mashoga wanawake, mashoga wanaume, waliobadilisha jinsia, wenye jinsia isiyo bayana, na wana-LGBTIQ+ wengine huenda wakaathiriwa na dhuluma kama hizo.
Ndoa za lazima na ukeketaji wa wanawake pia ni dhuluma na haziruhusiwi. Jamii ina jukumu la kulinda na kuwatunza watu wote wanaodhulumiwa, na kuhakikisha kuwa kila mtu anaweza kushiriki na kujumuishwa katika jamii kwa ujumla.
"Vurugu za kinyumbani ni kosa kubwa la jinai, ukiukaji wa haki za kimsingi za binadamu na tatizo kwa ustawi wa jamii."
Chanzo: Maisha bila vurugu, Mpango wa Utekelezaji dhidi ya Vurugu za Kinyumbani 2014-2017, Wizara ya Sheria na Usalama wa Umma
Mtandao
Jadilianeni pamoja
- Jadili tofauti kati ya vurugu za nyumbani na aina zingine za vurugu.
- Je, ni sababu ipi huenda ikamfanya mtu kutumia vurugu dhidi ya familia yake?
- Je, ni sababu ipi humpelekea mtu kuendelea kuishi na mwenzi wake anayetumia vurugu?
- Je, mitazamo kuhusu vurugu huenda ikawa ni tofauti katika tamaduni mbalimbali?
- Je, wanafamilia hufanyaje katika familia ambapo kuna vurugu?
Chagua jibu sahihi
Je, sheria za Norwe zinasema nini kuhusiana na vurugu?
Chagua jibu sahihi
Je, kuna aina gani za vurugu? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.
Kamilisha sentensi
Jamii hairuhusu aina yoyote ya vurugu...
Kamilisha sentensi
Vurugu za kinyumbani...
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?