Dini na misimamo mingine ya kifalsafa
Dini na misimamo mingine ya kifalsafa
Norwe ni jamii yenye tamaduni nyingi na isiyoongozwa na dini. Jamii isiyoongozwa na dini inamaanisha kuwa dini sio kigezo muhimu. Dini haizingatiwi na watu binafsi na haitumiki katika kutunga sheria za nchi. Mitazamo ya Wanorwe kuhusu dini imebadilika sana katika vizazi kadhaa vilivyopita. Dini ilikuwa ikitawala maisha ya watu kwa kiwango kikubwa. Leo, Wanorwe wengi hawazingatii dini sana, ingawa watu wengi huenda kanisani kwa ajili ya matukio muhimu kama vile ubatizo, kipaimara, harusi na mazishi.
Hadi mwaka wa 2012, Uprotestanti ndiyo ilikuwa dini rasmi nchini Norwe, na Kanisa la Norwe ndilo lilikuwa kanisa tawala. Kabla ya mwaka wa 1845, ilikuwa kinyume cha sheria kwa Wanorwe kuasi kanisa tawala, na mnamo 1850 iliruhusiwa kisheria kuanzisha jumuiya zisizo za Kikristo nchini Norwe. Hivyo, hakuna kanisa tawala au dini rasmi nchini Norwe. Lakini idadi kubwa ya wakazi wa Norway bado ni washiriki wa Kanisa la Norway. Waliosalia wamegawanywa miongoni mwa jamii zingine za kidini, au sio wa jamii yoyote ya kidini hata kidogo.
Kuna uhuru kamili wa kidini nchini Norwe. Hii inamaanisha kuwa unaweza kuwa mfuasi wa dini yoyote ile bila kuogopa kuteswa au kuadhibiwa. Pia inamaanisha kwamba kila mtu yuko huru kujiamulia dini anayopendelea. Na, muhimu pia, inamaanisha kuwa kila mtu yuko huru kuamua kutojihusisha na dini yoyote.
Dini na jamii mbalimbali zinaweza kupata msaada wa kifedha kutoka kwa manispaa na serikali kuu. Dini zilizosajiliwa, na jamii zenye mitazamo mbalimbali ya kifalsafa hupokea kiwango sawa cha fedha kwa kila mshirika kama vile Kanisa la Norwe.
Jadilianeni pamoja
- Je, dini imeathiri vipi maisha ya watu nchini Norwe hivi leo? Je, hali ikoje katika nchi zingine unazozijua?
- Je, ni vyema au si vyema kwa jamii kutoongozwa na dini?
- Je, dini tofauti zinaingiliana vipi leo nchini Norwe ikizingatiwa kuwa kuna tamaduni mbalimbali?
- Kumekuwepo na uhasama kati ya dini tofauti wakati mwingine. Je, hali ikoje leo, nchini Norwe na katika mataifa mengine duniani?
- Je, ni muhimu na unafaa kuonyesha msimamo wako wa kidini kupitia mavazi yako, mapambo na tabia?
Wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana kazini, Kåre alielezea kuhusu ubatizo wake uliofanyika siku iliyotangulia. "Kwaya iliimba vizuri, naye kuhani akahubiri vyema! Niliguswa sana." "Sikujua wewe ni mfuata dini?", mwenzake alisema. "La, siko hivyo. Lakini bado kuna kitu kuhusiana na hali, mila na desturi."
- Japo dini sio muhimu sana kwa Wanorwe wengi hivi leo, wengi wao hufanyia ndoa kanisani, huwabatiza watoto wao hukohuko na kadhalika. Jadili uhusiano uliopo kati ya dini na utamaduni.
Chagua jibu sahihi
Je, nini maana ya jamii kutoongozwa na dini?
Chagua jibu sahihi
Je, Wanorwe wanajihusisha vipi na dini?
Chagua jibu sahihi
Je, dini rasmi ilikuwa ipi nchini Norwe kufikia mwaka wa 2012?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?