Maisha nchini Norwe
Tazama filamu
Hali ya maisha ukiwa na watoto wachanga
- Je, kuna uhusiano na tofauti gani kati ya hali ya maisha ya mtu katika nchi yako na maisha ya Mnorwe hapa Norwe?
- Je, maisha yako yataathirika vipi kwa kuwa unaishi Norwe? Ni nini huenda kitabadilika?
Watu nchini Norwe kawaida huishi maisha tofauti. Hakuna watu wawili ambao maisha yao yanafanana. Hata hivyo, tuna takwimu za idadi ya watu wanaoishi nchini Norwe.
- Kila mwaka, zaidi ya watoto 50,000 huzaliwa nchini Norwei, na kwa wastani, kila mwanamke hupata watoto 1.4 (2023).
- Kwa wastani, wanawake Wanorwe huwa na miaka 30 wanapopata mtoto wa kwanza.
- Sio kawaida kwa wavulana kutahiriwa nchini Norway. Hata hivyo, tohara ya wasichana imepigwa marufuku kabisa. Hukumu ya kumpasha msichana tohara, au kuhusika katika kitendo hicho, ni kifungo cha hadi miaka 15. Inaweza pia kupelekea mtu kufukuzwa kutoka Norwe.
- Wazazi ambao wameajiriwa wana haki ya kupewa "msaada wa kifedha kwa wazazi" ya wiki 61 kwa jumla kuhusiana na kuzaliwa kwa mtoto (1.7.2024). Unaweza kupata maelezo kuhusu msaada wa kifedha kwa wazazi kwenye tovuti ya NAV.
Shule za chekechea, ruzuku ya utunzaji wa watoto na mafao ya watoto
Wazazi hulipa kiasi fulani ili watoto wao wajiunge na chekechea. Wazazi walio na watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja na miaka miwili hupokea ruzuku ya utunzaji wa watoto ikiwa mtoto haendi chekechea. Wazazi pia hupokea fedha zinazotolewa kwa ajili ya watoto, hadi mtoto atakapofikisha umri wa miaka 18.
Mtandao
Jadilianeni pamoja
- Je, kwa nini watoto wengi nchini Norwe huenda shule za chekechea?
- Jadili uhusiano kati ya shule za chekechea na ukuzaji wa lugha.
- Je, kwa nini familia zilizo na watoto wachanga hupokea ruzuku ya utunzaji wa watoto (kontantstøtte) na fedha zinazotolewa kwa ajili ya watoto?
Umri wa kuwa shuleni na ujana
Hapa Norwei, watoto huenda shule ya msingi (darasa la 1 hadi 7) na shule ya sekondari (darasa la 8 hadi 10). Zaidi ya asilimia 70 ya watoto katika darasa la 1 hadi 4 hushiriki katika shughuli za shule za wakati wa mapumziko (SFO), kabla na baada ya shule (2023-2024). Mpango huu wa shule ni wa hiari. Hakuna kulipa karo shuleni, lakini, kama sheria, wazazi huwalipia watoto wao ili kuhudhuria shughuli zinazofanywa na shule wakati wa mapumziko.
Watoto wengi nchini Norwe hushiriki katika shughuli moja au zaidi za wakati wa mapumziko. Shughuli nyingi hufanywa na wazazi kwa hiari. Wazazi hawalipwi kushiriki.
Karibu vijana wote huenda shule ya sekondari baada ya kuhitimisha masomo katika shule ya kati. Karibu nusu yao huchagua kozi ya masomo ya jumla, nao nusu waliosalia huchagua kozi ya kiufundi. Karibu asilimia 80 ya wanafunzi katika shule ya sekondari hukamilisha masomo yao.
Umri wa kuwa mtu mzima nchini Norwe ni miaka 18. Watu wana haki ya kujiamulia wenyewe. Watu ambao wamefikisha umri wa kuwa watu wazima wanaweza kupiga kura na kufanya mtihani wa udereva. Vijana wengi huondoka nyumbani kwenda chuo au chuo kikuu, au kufanya kazi, wakiwa miaka ishirini. Idadi kubwa ya wanafunzi hupata mkopo wa wanafunzi na hufanya kazi wakiendelea na masomo yao. Wengi wana mikopo ya wanafunzi ya zaidi ya NOK 300,000 wanapomaliza masomo yao.
Jadilianeni pamoja
- Je, mpango wa shughuli zinazofanywa na shule wakati wa mapumziko zina faida gani?
- Je, wewe na familia yako mngependa kufanya shughuli gani wakati wa mapumziko nchini Norwe?
- Je, kufikisha umri wa kuwa mtu mzima kunamaanisha nini?
- Je, unajua umri wa kuwa mtu mzima ni gani katika nchi zingine unazozijua?
- Je, maoni yako ni gani kuhusu mfumo wa mikopo ya wanafunzi?
Utu uzima na kustaafu
Wastani wa umri wa ndoa ya kwanza ni kati ya miaka thelathini na arobaini, kwa wanaume na wanawake. Wapenzi wengi nchini Norwe huishi pamoja kwa muda kabla ya kuoana.
Ni kawaida kwa wanaume na wanawake kufanya kazi nje ya nyumbani na kwa wanawake na wanaume kushiriki kazi za nyumbani. Hata hivyo, wanawake hutumia muda mwingi kuliko wanaume kila wiki kufanya kazi za nyumbani. Ni kawaida kukopa benki pesa ili kununua nyumba na gari. Kwa wastani, familia ya kawaida yenye watoto wana mkopo wa nyumba wa zaidi ya NOK milioni 2.
Umri wa kustaafu nchini Norwe ni 67 kwa wanaume na wanawake. Watu wengi wana chaguo la kustaafu na kupokea pensheni kabla ya umri huu, na kuna wengine huamua kufanya kazi hadi watakapofikisha miaka 70. Pensheni ni pesa unazolipwa unapostaafu. Pensheni yako hutegemea mshahara wako. Watu ambao hawajaajiriwa, kama vile wake wa nyumbani, pia hupokea pensheni wakiwa umri wa miaka 67.
Watu wengi wakonge nchini Norwe wanaendeleza shughuli maishani. Wanahusika katika mashirika tofauti, na hutumia muda mwingi na familia na marafiki. Watu wazee mara nyingi wana pesa nyingi. Wengi wao wamelipa madeni yao na hawahitaji kushughulikia mahitaji ya watoto wao.
Wastaafu wengi hujishughulikia nyumbani bila usaidizi kutoka kwa mamlaka ya eneo lao. Idadi ndogo ya wastaafu hupokea huduma za afya nyumbani kwao na/au usaidizi kuhusiana na shughuli zao za kila siku.
Watu wengi wanaofariki nchini Norwe huzikwa kwenye makaburi, lakini wengi wameanza kupendelea kuchomwa. Makaburi mengine yana maeneo maalum yaliyotengewa dini tofauti. Ikiwa mtu anayefariki ana mwenzi na watoto, wanarithi mali ya aliyeaga. Wanawake na wanaume wana haki sawa za urithi. Urithi unadhibitiwa chini ya sheria husika. Kama sehemu ya urithi, inawezekana pia kwa mwenye mali kuandika matarajio yake ya kugawanya mali.
Jadilianeni pamoja
- Jadili uhusiano uliopo kati ya mshahara na pensheni.
- Je, ukilinganisha na wastaafu katika nchi unazozijua, hali ya wanaopokea pensheni nchini Norwe ikoje?
- Je, maoni yako ni gani kuhusu makaburi yaliyo na maeneo maalum yaliyotengewa dini tofauti?
Chagua jibu sahihi
Je, watoto wangapi huzaliwa nchini Norwe kila mwaka?
Chagua jibu sahihi
Je, kwa wastani, wanawake Wanorwe huwa na miaka mingapi wanapopata mtoto wa kwanza?
Chagua jibu sahihi
Je, umri wa kustaafu ni upi nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Bofya picha
Bofya ili uchague mtu sahihi kwenye picha. Je, umri wa kuwa mtu mzima nchini Norwe ni upi?