Mazingira na maliasili
Tazama filamu
Mazingira na maliasili
Katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, Norwe imekuwa mojawapo ya nchi tajiri zaidi ulimwenguni. Utajiri huu umetokana na wingi wa maliasili na jinsi Wanorwe wamejifunza kuzitumia. Maliasili inayopatikana kwa wingi nchini Norwe ni samaki, misitu na mafuta. Pia, kuna maji kwa wingi katika mito na maporomoko ya maji nchini Norwe, yanatumiwa kuzalisha umeme. Katika miaka ya hivi majuzi, tabo za upepo pia zilianza kutumika kuzalisha nguvu za umeme.
Mafuta yalipatikana mara ya kwanza nchini Norwe katika Bahari ya Kaskazini mwishoni mwa miaka ya 1960. Mafuta yamekuwa ya umuhimu mkubwa kwa uchumi wa Norwe.
Norwe huuza bidhaa nyingi zinazotokana na maliasili. Vyuma ni bidhaa muhimu zinazouzwa nje ya nchi, hasa aluminiamu. Sekta ya uundaji chuma inahitaji umeme mwingi, na umeme unaozalishwa kupitia maji umewezesha utengenezaji wa chuma kwa kiasi kikubwa. Samaki pia ni maliasili muhimu nchini Norwe. Tunauza samaki katika nchi nyingi, na uuzaji huu unaongezeka kila mwaka. Norwe ina misitu mingi. Baadhi ya mbao hutayarishwa kwa njia maalum. Mbao hutumiwa, kati ya mambo mengine, kutengeneza karatasi na vifaa vya ujenzi. Baadhi ya mbao pia hupelekwa nchi zingine.
Mazingira na maisha katika mandhari ya nje
Mazingira yenyewe pia ni rasilimali. Watalii kutoka kote ulimwenguni huja kuona Jua la Usiku wa Manane na mabonde marefu yenye maji. Watu wengi wanaoishi Norwe wanapenda kupumzika na kujivinjari kwa kuzuru mandhari asili. Popote ambapo watu wanaishi nchini Norwe, mazingira asili hupatikana karibu na mtu yeyote anaweza kwenda kokote. Hii inajulikana kama haki ya kutumia ardhi ya umma. Katika sehemu ambako watu hawaishi (fukwe, sehemu zenye majimaji, misitu na milima), unaweza kwenda popote kwa miguu au kwa kutumia mashua ndogo kisha upumzike kokote. Unaweza kulala nje au katika hema, lakini sharti ufanye hivyo angalau mita 150 kutoka nyumba au kijumba kilicho karibu. Ikiwa ungependa kukaa mahali pamoja zaidi ya siku mbili, unapaswa kupata idhini ya mmiliki wa ardhi hiyo.
Haki ya kutumia ardhi ya umma pia inaambatana na majukumu. Hupaswi kuwadhuru wanyama au kuharibu mazingira. Unafaa kusafisha sehemu uliyotumia na hupaswi kuacha takataka yoyote. Pia unapaswa kuwa mwangalifu unapowasha moto. Kuwasha moto msituni au karibu na msitu ni marufuku kuanzia tarehe 15 Aprili hadi tarehe 15 Septemba. Unaruhusiwa kutumia kichoma-nyama kinachotumika mara moja, lakini unapaswa kuwa makini sana.
Unaweza kuchuma beri, uyoga na maua katika maeneo mengi. Wanorwe wengi huvua samaki au kuwinda wakati wao wa ziada. Kawaida, unahitaji kulipia kibali cha kuvua samaki katika mito na ziwa.
Jadilianeni pamoja
- Je, nchi yako ina raslimali zipi, na zinatumikaje?
- Jadili kuhusu manufaa na changamoto za uchimbaji wa mafuta, na uzalishaji umeme kwa kutumia upepo.
- Jadili kuhusu haki ya kutumia ardhi ya umma. Je, haki hii ipo katika nchi zingine unazojua?
Chagua jibu sahihi
Je, ni bidhaa ipi ambayo Norwe huuza katika nchi zingine kwa wingi?
Chagua jibu sahihi
Je, haki ya kuzuru mandhari asili hujulikana kama?
Chagua jibu sahihi
Je, una majukumu gani unapozuru mandhari asili?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Bofya picha
Bofya sehemu sahihi kwenye picha. Je, huruhusiwi kufanya nini msituni au karibu na msitu kati ya tarehe 15 Aprili hadi tarehe 15 Septemba?