Sheria na masharti kazini
Sheria na masharti kazini
Kuna sheria, masharti na makubaliano ya kazini ambayo waajiri na wafanyakazi sharti wazingatie.
Wanachama wa Storting wanapitisha sheria, nao waajiri na wafanyakazi wanafanya makubaliano kupitia mashirika yao. Sheria zinatumika kwa waajiri na wafanyakazi wote, nayo makubaliano ya pamoja yanatumika tu kwa sekta mahususi zilizobuni mikataba hiyo.
Sheria za kazini
Waajiri na waajiriwa wote wanapaswa kuzingatia Sheria za Kazini. Pamoja na mengine, Sheria ya kazini inashughulikia:
- kuajiri na mikataba
- saa za kazi
- kutofika kazini
- kushughulikia afya, usalama na mazingira (HMS)
Mwajiri anawajibikia mazingira ya kazini, naye mfanyakazi anahitajika:
- kusaidia kukuza mazingira yanayofaa kazini
- kusaidia kutekeleza hatua zilizochukuliwa kuboresha mazingira ya kazini
- kushiriki katika mchakato wa usalama na mazingira iliyopangwa kazini
Sheria ya likizo
Pamoja na mengine, Sheria ya likizo inashughulikia:
- muda unaopaswa kwenda likizo
- ni lini unapaswa kwenda likizo
- likizo wakati wa vipindi vya kutoa notisi
- ugonjwa wakati wa likizo
- malipo ya likizo
- Wafanyakazi nchini Norwe wana haki ya kwenda likizo ya wiki nne na likizo ya siku moja kila mwaka, lakini baadhi ya waajiriwa wana likizo ya wiki tano.
- Hatupokei malipo mengine wakati wa likizo, kando na malipo ya likizo.
- Kiasi cha malipo ya likizo unachopata kinategemea mapato yako ya mwaka uliopita.
Jadilianeni pamoja
- Je, ni nani aliyebuni sheria za kazi nchini Norwe?
- Je, sheria ziliibuka vipi?
- Kwa nini ni muhimu waajiri na waajiriwa kufahamu sheria na masharti?
- Je, sheria na masharti ni chanzo cha uhuru au vizuizi?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani anayepaswa kuzingatia Sheria za Kazini?
Chagua jibu sahihi
Je, unastahili kwenda likizo ya siku ngapi kwa mwaka nchini Norwe?
Kamilisha sentensi
Kiasi cha malipo ya likizo unachopata kinategemea...
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?