Uzingatiaji wa masilahi
Uzingatiaji wa masilahi
Norwe ni nchi inayojali maslahi ya watu na ustawi wake unategemea usawa. Hii inamaanisha kuwa watu wote ni muhimu na kwamba kila mtu ana nafasi ya kuishi maisha mazuri. Serikali kuu na manispaa zinawajibika zaidi katika utoaji wa faida za maslahi. Tunaiita Norwe nchi ya maslahi.
Nchi kujali maslahi ya watu wake ni jambo zito. Nchi ya Norwe ni nchi inayojali maslahi ya watu wake na imejengwa hatua kwa hatua katika kipindi cha miaka 100. Mipango yote ya mafao hugharimu pesa nyingi. Wanasiasa huamua mipango ya mafao itakayotekelezwa. Hivyo uamuzi wao unaweza kubadilika kutegemea vyama vilivyo madarakani na hali ya kifedha iliyopo.
Nchi inayojali maslahi ya watu wake inategemea watu wengi iwezekanavyo kufanya kazi na kulipa ushuru. Watu wengi pia wanapendelea kujikimu na kujitegemea. Hata hivyo, nchi inayojali maslahi ya watu wake inaweza kutoa msaada wa kifedha kwa wale wanaohitaji.
Mifano ya mipango ya maslahi:
- malipo ya wagonjwa
- mafao kwa wasio na ajira
- mafao ya mwanzo
- elimu ya bila malipo
- huduma ya bila malipo hospitalini
- mafao ya watoto
Matumizi ya mfumo wa maslahi unategemea sana uaminifu. Serikali kuu na watu wanaaminiana. Watu wanaamini kuwa serikali kuu itawasaidia inapohitajika, nayo serikali kuu inaamini kuwa watu hawatatumia vibaya mfumo wa maslahi.
NAV
Kila manispaa nchini Norwe ina ofisi ya NAV. Ofisi ya NAV inaweza kutusaidia ikiwa tunahitaji kutimiza masharti ya kupata kazi au ikiwa tunahitaji msaada wa kifedha wakati wa magonjwa au magumu. Pia, NAV inawajibikia faida zote za Bima ya Kitaifa nchini Norwe. NAV pia inawajibika kwa faida za usalama wa jamii, mafao kwa wasio na ajira, mafao ya magonjwa, pensheni, mafao ya watoto na mpango wa mafao ya pesa taslimu, miongoni mwa nyinginezo.
NAV inasimamia takriban thuluthi moja ya bajeti ya kitaifa na ina wafanyakazi karibu 22,000.
Uzingatiaji wa maslahi ya watu huzalisha nafasi za kazi
Nchi inayozingatia maslahi ya watu wake inahitaji wafanyakazi wengi. Takriban asilimia 30 ya walioajiriwa nchini Norwe leo wanafanya kazi katika sekta ya umma. Nchi ya Norwe inazingatia maslahi ya watu wake na inahitaji wafanyakazi mbalimbali ili kustawi.
Mifano inajumuisha:
- walimu, wafanyakazi wa ofisi, wafanyakazi wengine wa shule
- madaktari, wauguzi, wahudumu wa afya, wafanyakazi wa ofisi, wasafishaji na wafanyakazi wengine katika hospitali na makao ya wakongwe
- wachunguzi, wafanyakazi wa ofisi na wafanyakazi wengine wa NAV
Jadilianeni pamoja
- Je, usawa ni nini? Je, maslahi ni nini? Je, nini maana ya maisha mazuri?
- Eleza kuhusu mfumo wa maslahi nchini Norwe.
- Jadili kuhusu umuhimu wa NAV kuhusiana na maslahi nchini Norwe.
- NAV inasimamia takriban thuluthi moja ya bajeti ya kitaifa ya Norwe. Je, hii inatueleza nini kuhusu nchi ya Norwe? Je, pesa hizo zinatoka wapi?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani aliye na jukumu kuu la kutoa mafao ya maslahi kwa wanaoishi Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, mifano ya mipango ya maslahi ni ipi? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.
Chagua jibu sahihi
Je, NAV ina majukumu yepi? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua picha sahihi
Je, ni kazi gani za kitaalam tunazozipata katika sekta ya umma? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.