Ukweli kuhusu Norwe
Tazama filamu
Ukweli kuhusu Norwe
- Norwe ni ya utawala wa kifalme. Mfalme Harald ndiye mkuu wa nchi. Utawala hurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
- Norwe ina watu milioni 5.5 (01.01.2024). Karibu asilimia 75 ya wakaazi wanaishi pwani. Nusu ya wakaazi wanaishi Kusini-Mashariki mwa Norwe.
- Kuna lugha mbili rasmi za kitaifa nchini Norwe, Kinorwe na Kisami. Kuna lugha mbili za Kinorwe zilizoandikwa, Bokmål na Nynorsk.
- Ina ukubwa wa kilomita 385,178 mraba. India ni karibu mara kumi kwa ukubwa.
- Norwe inapakana na nchi ya Uswidi, Ufini na Urusi.
- Mji wake mkuu ni Oslo. Oslo ndio mji mkubwa zaidi nchini Norwe na ina idadi ya watu takriban 700,000 (kufikia mwaka wa 2024).
- Miji minne mikubwa ni Oslo, Bergen, Trondheim na Stavanger.
- Lindesnes ndiyo sehemu ya kusini kabisa nchini Norwe.
- Knivskjelodden inayopatikana Nordkapp (North Cape) ndiyo sehemu ya kaskazini zaidi nchini Norwe.
- Svalbard ni kikundi cha visiwa vya nchi ya Norwe.
- Norwe imegawanywa katika kaunti 15.
- Norwe ina manispaa 356.
Chanzo: www.ssb.no, www.fn.no, www.oslo.kommune.no
Mandhari
Norwe ina milima mikubwa, na pia ina misitu mingi. Misitu mikubwa na milima ni jangwa na watu hawaishi huko. Baadhi ya milima ina theluji na barafu isiyoyeyuka
Pwani ndefu ya Norwe ina urefu wa kilomita 25,148. Urefu huo unazidi umbali kutoka Ncha ya Kaskazini hadi Ncha ya Kusini! Mazingira ya pwani ni tofauti kutoka kusini hadi kaskazini. Katika maeneo mengi, ghuba kubwa na ndogo na mabonde marefu yenye maji huenda umbali mkubwa. Pia kuna karibu visiwa 50,000 kwenye mwambao wa pwani, lakini ni visiwa vichache tu vina makaazi ya watu. Baadhi ya visiwa vimeunganishwa na bara kupitia daraja au handaki, nazo feri zinatumika kwenye visiwa vingine
Unaweza kusafiri kwa urahisi nchini Norwe. Usafiri wa umma umedumishwa vizuri kabisa. Unaweza kusafiri kwa gari, basi, treni, mashua au ndege.
Chanzo: SSB (Ofisi ya Takwimu ya Norway)
Gundua kuhusu mandhari ya Norwe
Hali ya hewa
Norwe ina misimu minne: majira ya baridi, masika, majira ya joto na vuli.
Norwe iko upande wa kaskazini. Hata hivyo, hakuna baridi kali kama inavyodhaniwa. Hii ni kutokana na mawimbi ya Gulf Stream. Mawimbi ya Gulf Stream huleta maji mengi yenye joto kutoka sehemu za kusini mwa Atlantiki hadi pwani ya Norwe. Hii inamaanisha kuwa kiwango cha joto nchini Norwe kiko juu ikilinganishwa na latitudo yake.
Hali ya hewa ni tofauti katika sehemu mbalimbali. Pia kuna tofauti kubwa kati ya hali ya hewa ya pwani na bara. Misimu ya baridi hukaa muda mrefu, baridi huwa kali na giza huwepo Kaskazini mwa Norwe. Misimu ya joto ni mifupi, lakini kuwepo kwa Jua la Usiku wa Manane kunamaanisha kuwa majira haya ni ya mwangaza na ya kupendeza. Kuna barafu nyingi kwenye nchi kavu Kusini mwa Norwe, lakini barafu ni kidogo sehemu za pwani. Kusini mwa Norwe na Mashariki mwa Norwe kawaida huwa na majira ya joto ya kupendeza na hakuna baridi. Majira ya masika huja mapema Magharibi mwa Norwe. Mvua hunyesha zaidi upande wa Magharibi kuliko Mashariki mwa Norwe. Huenda kukawa na dhoruba pwani nzima kuanzia Magharibi mwa Norwe kuelekea kaskazini hadi msimu wa vuli.
Nchini Norwe, inachukuliwa kuwa kuna joto viwango vinapofikia nyuzi joto 25. Kiwango cha joto cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Norwe kilikuwa nyuzi joto 35.6. Kilirekodiwa mjini Nesbyen Mashariki mwa Norwe mnamo tarehe 20 Juni, 1970. Kiwango cha joto cha chini zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Norwe kilikuwa chini ya sufuri kwa nyuzi joto 51.4. Kilirekodiwa mjini Karasjok Kaskazini mwa Norwe mnamo tarehe 1 Januari 1886.
Jadilianeni pamoja
- Eleza kuhusu nchi unayoifahamu vizuri: Hali ya hewa ikoje? Watu wanaishi wapi? Je, mazingira na hali ya hewa zinaathiri vipi maisha ya watu?
- Jadili kuhusu jinsi hali ya hewa inavyoathiri hali ya ajira na maendeleo ya kijamii katika nchi fulani.
- Je, hali ya hewa na joto iko vipi katika sehemu ya Norwe unakoishi?
- Je, kuna fursa zipi na vizuizi vipi nchini Norwe kutokana na hali ya hewa?
Nyanya: Kumenyesha siku kadhaa mfululizo. Je, unadhani mvua itakwisha lini?
Mama: Ni vigumu kujua hilo. Lakini taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwenye redio zilisema kuwa hali ya hewa itakuwa bora wikendi.
Binti: Unapenda kuzungumzia hali ya hewa kila wakati!
Mama: Wanorwe wanapenda kuzungumzia hali ya hewa.
Kwa nini Wanorwe wanapenda kuzungumza kuhusu hali ya hewa?
Chagua jibu sahihi
Je, kuna lugha ngapi rasmi za kitaifa nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Mto mrefu zaidi nchini Norwe unaitwaje?
Chagua jibu sahihi
Je, kiwango cha joto cha chini zaidi kurekodiwa nchini Norwe kilikuwa nyuzi ngapi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua picha sahihi.
Je, ni picha ipi inaonyesha majira ya vuli?