Kusoma Kinorwe
Kusoma Kinorwe
Lengo ni kwamba kila mtu anayeishi Norwe afahamu Kinorwe. Kuzungumza lugha moja husaidia kukuza jamii na kuhimiza utangamano. Kwa kutegemea idhini ya ukaaji ambayo wageni wamepewa nchini Norwe, wanaokaa nchini humu watakuwa na chaguo tofauti za kusoma Kinorwe. Wengine wana haki ya kusoma Kinorwe bila malipo na wanahitajika kukamilisha masomo. Wengine wanapaswa kusoma Kinorwe lakini wanahitajika kujilipia wenyewe.
Muda wa kusoma Kinorwe kwa wale ambao wana haki na wajibu wa kujifunza unategemea kiwango cha lugha ambacho kimebainishwa kwa anayejifunza. Viwango vimegawanywa katika A1, A2, B1 na B2 kulingana na Mfumo wa Ulaya wa Marejeleo ya Lugha.
Kiwango cha kujifunza lugha kwa kawaida kinategemea kiwango cha elimu cha mtu anapowasili nchini Norwe. Kiwango cha elimu kikiwa juu, kiwango cha kujifunza kinakuwa juu pia. Kiwango cha kujifunza lugha kinaweza kubadilishwa mtu anapoendelea, kutegemea hatua anazopiga. Sharti uhitimishe masomo yote ya lugha ya Kinorwe ndani ya miaka mitatu. Kwa wenye elimu ya juu au waliofika kiwango cha shule ya upili, muda wa kujifunza Kinorwe ni miezi 18. Unapokamilisha masomo hayo unafanya mtihani kwa Kinorwe ili kupata cheti cha kuonyesha kiwango cha lugha ambacho umefikia.
Je, mtu hujifunzaje Kinorwe?
Kuna njia nyingi za kujifunza lugha na zipo sehemu mbalimbali ambapo unaweza kujifunza. Watu wengi hufanya kozi ya lugha ya Kinorwe kwa sababu wanataka masomo yenye utaratibu na ya kimfumo. Wanaoishi Norwe pia huzungukwa kila wakati na lugha ya Kinorwe. Watasikia watu wakiongea Kinorwe kwenye basi na dukani, na watasikia na kuona kwenye televisheni, redio, gazeti na mitandao ya kijamii. Watu ambao wana watoto watawasikia wakizungumza Kinorwe na marafiki wao, na lazima wazungumze Kinorwe kwa wafanyakazi au walimu wa chekechea.
Watu wenye hamu na umakini watapata fursa nyingi za kufanya mazoezi ya Kinorwe kila siku. Wale wanaokubali fursa ya lugha kazini wanapata fursa ya kipekee ya kujifunza lugha hiyo katika mazingira asili.
Chanzo: IMDi
Jadilianeni pamoja
- Jadilianeni pamoja kuhusu fursa unazopata za kusikia lugha ya Kinorwe kila siku.
- Kwa nini ni muhimu kwa kila mtu anayeishi Norwe kuelewa na kuzungumza Kinorwe?
- Je, unawezaje kujifunza lugha mwenyewe?
Chagua jibu sahihi
Je, viwango vya lugha hubainishwa vipi katika Mfumo wa Lugha wa Ulaya?
Kamilisha sentensi
Sharti uhitimishe masomo yote ya lugha ya Kinorwe ndani ya miaka mitatu. Kwa wale waliofika shule ya upili au wenye elimu ya juu, muda wa kukamilisha ni
Chagua jibu sahihi
Kimsingi, kiwango cha kujifunza lugha kwa kawaida kinategemea kiwango cha elimu cha mtu anapowasili nchini Norwe. Hii inamaanisha nini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?