Desturi potovu za kijamii
Desturi potovu za kijamii
Desturi za kijamii ni neno linalotumiwa kurejelea mfumo unaohusiana na tabia na mtindo wa maisha ya mtu binafsi. Kwa mfano, wazazi huweka mfumo unaozunguka maisha ya watoto wao wanapowalea, na jamii huweka mfumo wa tabia inayokubalika kupitia sheria na kanuni zilizoandikwa na ambazo hazijaandikwa.
Wakati mwingine, watoto na vijana na hata watu wazima wanaweza kuchukulia kuwa sheria wanazowekewa na familia zao ni kali sana. Sheria hizo huchukuliwa kuwa zisizofaa na desturi za kijamii huonekana kama zinazoumiza. Desturi ambazo wazazi au jamaa wengine wa karibu huweka, huenda pia zikakinzana na zile zinazochukuliwa na jamii kuwa za kawaida. Desturi potovu za kijamii zinaweza kumnyima mtu uhuru wa kibinafsi na haki ya kuishi maisha ya kujitegemea. Desturi potovu za kijamii zinaweza kuwazuia watoto na vijana kushirikishwa katika jamii ya Norwe.
Jadilianeni pamoja
Merhet ana umri wa miaka 14 na yuko shule ya kati. Alipokuwa mtoto, aliishi maisha huru na wazazi wake walimwekea mipaka kadhaa. Sasa amebaleghe, amegundua kuwa wazazi wake wamekuwa wakali zaidi. Haruhusiwi kwenda nyumbani na marafiki, na anatarajiwa kurudi nyumbani moja kwa moja baada ya shule. Amelazimika kuacha kucheza mpira wa mikono kwa sababu baba yake hapendi avalie kaptula anapocheza. Mama yake huangalia simu yake kila usiku ili kuona wanaomtumia ujumbe.
Kaka yake anamzidi umri kwa miaka miwili. Wazazi sio wakali kwake. Hili limemkasirisha Merhet na anafikiria kuwa wazazi wake wameacha kumwamini. Je, wanadhani atafanya kitu kibaya wasipomfuatilia kila wakati?
Jadili hali ya Merhet.
- Je, wazazi wake wanachukulia vipi hali hiyo?
- Je, ufuatiliaji huu wa wazazi unaweza kusababisha nini?
- Je, Merhet na wazazi wake wanawezaje kuboresha maisha yao ya kila siku?
Miaka miwili baadaye:
Merhet yuko shule ya upili. Maisha yake yamekuwa magumu zaidi. Maisha yake ya kila siku ni tofauti kabisa na marafiki zake Wanorwe anaosoma nao shuleni. Wasichana wengine katika darasa lake mara nyingi hukutana baada ya shule na kufanya pamoja mambo ya kufurahisha. Wanalala nyumbani kwa kila mmoja wakati wa wikendi na kuzungumza kuhusu wavulana na mitindo ya mavazi. Merhet anahisi kuwa yeye si sehemu ya jamii ya Norwe. Japo anaipenda familia yake, anahisi kuwa hana uhuru wake na amenaswa. Amesikia kwamba yupo mshauri wa wachache shuleni anakosoma. Je, anapaswa kuzungumza naye?
- Je, ungemshauri Merhet afanye nini?
Chagua jibu sahihi
Je, desturi za kijamii ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, desturi potovu za kijamii ni nini?
Kamilisha sentensi
Watu wanapochukulia kuwa sheria zinazowekwa na familia zinaumiza sana,...
Kamilisha sentensi
Desturi potovu za kijamii zinaweza...
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?