Norwe ya hivi Leo
Norwe ya hivi Leo
Leo, Norwe ni nchi ya kisasa, yenye tamaduni nyingi. Kiwango cha maisha kiko juu na jamii inaongozwa na teknolojia ya kisasa. Norwe pia inajihusisha na mashirika ya kimataifa yanayoathiri sera zake, ikijumuisha Umoja wa Ulaya, NATO na EEA.
Ukimuuliza mtu yeyote kuhusu maadili ambayo ni muhimu katika jamii ya Norwe hivi leo, huenda akasema kwamba maadili muhimu zaidi ni usawa na uhuru wa kujiamulia mwenyewe.
Kama ilivyo katika nchi na jamii nyingi, kuna sheria nyingi nchini Norwe. Sheria zinategemea kwa kiasi kikubwa usawa kati ya watu, na huwapa watu haki nyingi. Tutaangalia sababu kadhaa hapa chini ambazo zimesaidia kuunda Norwe kuwa vile ilivyo leo. Vyama vikubwa vya kisiasa vimesaidia sana katika maendeleo ya Norwe ya leo. Miungano ya wafanyakazi na miungano ya wanawake imekuwa muhimu sana.
Muungano wa wafanyakazi
Chimbuko la muungano wa wafanyakazi wa Norwe ni la karne ya 17, lakini muungano ukawa na taratibu rasmi kufuatia nafasi za kazi kuongezeka viwandani kuanzia miaka ya 1880 na kuendelea. Muungano huu ulipata ushawishi mkubwa zaidi mwanzoni mwa miaka ya 1900. Jitihada za muungano wa wafanyakazi zimesababisha mazingira bora ya kufanyia kazi, ikiwemo kufanya kazi saa chache, usalama ulioboreshwa kazini, bima ya afya na haki ya msaada wa kifedha kwa watu wasio na ajira. Leo, karibu nusu ya wafanyakazi wote ni wanachama wa vyama vya wafanyakazi.
Muungano wa wanawake
Muungano wa wanawake umetetea haki za wanawake katika jamii na fursa sawa kwa wanaume na wanawake. Miungano ya wanawake ilikuwa maarufu nchini Norwe kuanzia miaka ya 1880, na wanawake huko Norwe walipata haki ya kupiga kura mnamo 1913.
Mapambano ya haki za wanawake yalifanyika tena katika miaka ya 1970. Sheria inayohusiana na Kuavya Mimba (Sheria ya Kuavya Mimba) ilipitishwa mnamo 1978. Pamoja na mambo mengine, sheria hii inawaruhusu wanawake kuavya mimba hadi wiki ya 13 ya ujauzito. Haki ya talaka, kupanga uzazi, kuavya mimba na haki ya wanawake kufanya maamuzi kuhusu miili yao zimekuwa masuala muhimu kwa harakati za wanawake.
Leo, wanaume na wanawake wana haki sawa za elimu na kazi, mali na urithi, afya na utunzaji. Jinsia ya mtu haitumiki tena kubaini haki na fursa za mtu huyo. Wapo wanaoamini kuwa itachukua muda kufikia usawa katika masuala fulani.
Mafuta
Katika miaka ya 1960, kampuni kadhaa zilitaka kutafuta mafuta na gesi katika pwani ya Norwe. Mafuta yalipatikana mara ya kwanza katika Bahari ya Kaskazini mnamo 1967, na Norwe imejikuza kuwa taifa la mafuta. Sekta ya mafuta imekuwa muhimu sana kwa uchumi wa Norwe. Sawa na umeme uliotokana na maji miaka 50 iliyopita, mafuta yalibakia kuwa mali ya umma. Kampuni za kibinafsi zinaweza kununua haki za utafutaji, uchimbaji na utengenezaji wa mafuta katika maeneo mahususi kwa muda mfupi. Leo, sekta ya mafuta ni suala tata nchini Norwe. Watu hawakubaliani kuhusu matokeo ya sekta hii kuhusiana na mazingira.
Jadilianeni pamoja
- Kabla ya 1850, karibu asilimia 15 ya watu walikuwa wakiishi mijini. Karibu mwaka wa 1900, asilimia 35 ya watu waliishi mjini, na leo takriban asilimia 80 ya watu nchini Norwe wanaishi katika miji. Je, hali iko vivyo hivyo katika nchi zingine unazojua?
- Jadili manufaa na athari za watu kuhamia mijini kutoka mashambani.
- Jadilianeni pamoja kuhusu umuhimu wa miungano ya wafanyakazi kwa maendeleo ya Norwe hivi leo. Je, hali iko vivyo hivyo katika nchi zingine unazojua?
- Jadilianeni pamoja kuhusu umuhimu wa miungano ya wanawake kwa maendeleo ya Norwe hivi leo. Je, hali iko vivyo hivyo katika nchi zingine unazojua?
- Jadilianeni pamoja kuhusu haki za wanawake huko Norwe na maeneo mengine ulimwenguni hapo awali na sasa.
- Je, kuna umuhimu wowote kwa Norwe kutokuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya?
- Kugunduliwa kwa mafuta na gesi katika Bahari ya Kaskazini mwishoni mwa miaka ya 1960 kumeifanya Norwe kuwa nchi tajiri. Hata hivyo, haki ya kupata elimu ya bila malipo, huduma ya afya bila malipo au kwa gharama ya chini, saa chache za kufanya kazi, bima ya afya nk. zilitokea kabla ya mafuta kugunduliwa. Jadilianeni pamoja kuhusu maadili ambayo ndio msingi wa haki hizi.
Chagua jibu sahihi
Je, asilimia ngapi ya wafanyakazi nchini Norwe wako katika vyama vya wafanyakazi hivi leo?
Chagua jibu sahihi
Je, mafuta yalipatikana lini katika Bahari ya Kaskazini?
Chagua jibu sahihi
Je, Sheria ya Kuavya Mimba, ya Mwaka wa 1978 inawaruhusu wanawake kufanya nini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?