Sheria kwa wakaaji
Sheria kwa wakaaji
Mhamiaji ni mtu aliyezaliwa nchi nyingine, lakini anaishi Norwe. Wahamiaji nchini Norwe wana haki na vibali mbalimbali vya ukaaji.
- Wahamiaji kutoka nchi za EU/EEA wanaweza kufanya kazi nchini Norwe bila kupokea kibali cha ukaaji, lakini sharti wajiandikishe kwa polisi. Mchakato huu hufanywa kidijitali.
- Wakimbizi waliohamishwa kutoka nchi waliyokimbilia huja Norwe kwa makubaliano na UNHCR (Umoja wa Mataifa). Wanapata kibali cha ukaaji wa muda wanapokuja Norwe.
- Mtu anayedhulumiwa katika nchi yao kwa sababu ya rangi, dini, utaifa, mwelekeo wa kijinsia au kisiasa, anaweza kupewa uhifadhi nchini Norwe. Wanaotafuta uhifadhi huja Norwe kuomba uhifadhi. Maombi yao yanaweza kukataliwa au kupewa hifadhi/idhini ya ukaaji kwa kuzingatia maslahi ya kibinadamu.
- Wanafamilia wa watu walio na idhini ya ukaaji nchini Norwe wanaweza kutuma ombi la kuungana na familia.
Watu ambao wamepewa uhifadhi/makao kwa sababu ya masuala ya kibinadamu, na wakimbizi waliohamishwa kutoka nchi waliyokimbilia, wanajulikana kama wakimbizi.
Watu hupewa kibali cha kukaa kwa muda kwa miaka yao mitatu au mitano ya kwanza nchini Norwe. Kibali kwa ujumla kinapaswa kutolewa upya kila mwaka. Baada ya miaka mitatu au mitano, unaweza kuomba kibali cha ukaaji wa kudumu. Baada ya miaka sita, saba au nane, unaweza kuomba uraia wa Norwe.
Chanzo: www.udi.no
Kwenye tovuti ya UDI, unaweza kujaza maelezo na kupokea mwongozo uliobinafsishwa. Maombi husika ya kazi yanaweza pia kutumwa kwa njia ya kidijitali hapa. Tovuti inapatikana katika lugha ya Kinorwe na Kiingereza.
Mtandao
Jadilianeni pamoja
- Je, ni nani hubaini wanaopaswa kuishi katika nchi fulani?
- Je, mtu yeyote anayetaka anaweza kuhamia nchi yako?
- Je, kwa nini idhini ya mkaazi haitolewi kwa kila mtu anayeihitaji nchini Norwe?
- Je, nchi ina jukumu gani kuhusu kupokea wakimbizi, na wakimbizi wenyewe wana jukumu gani?
Chagua jibu sahihi
Je, neno mhamiaji linamaanisha nini?
Chagua jibu sahihi
Je, wakaazi kutoka nchi za EU/EEA wanaweza kufanya kazi nchini Norwe bila kuomba kibali cha ukaaji?
Chagua jibu sahihi
Je, kwenye tovuti gani unaweza kujaza maelezo na kupata mwongozo maalum kuhusu ukaaji?
Chagua jibu sahihi
Je, wanafamilia wa watu walio na idhini ya ukaaji nchini Norwe wanaweza kutuma ombi lipi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?