Zama za Kati na Miungano
Zama za Kati na Miungano
Ukristo umefika Norwe
Kabla ya Ukristo kufika Norwe, ilikuwa ndiyo dini kuu kusini mwa Ulaya kwa muda mrefu. Olav Haraldsson alipouawa katika vita vya Stiklestad mnamo 1030, mwanawe aliomba usaidizi wa kanisa katika kumfanya baba yake kuwa mtakatifu. Polepole, wakuu na wakulima wenye usemi mkubwa walianza kuunga mkono na kufuata Ukristo. Watawala walipobadili dini na kuanza kufuata nyingine mpya, raia wengi wa kawaida walimfuata. Baada ya muda kanisa lilikuwa na ushawishi mkubwa. Watu walilipa ushuru kwa kanisa, na wengi wao pia waliipa kanisa mashamba yao. Dini ilikuwa muhimu sana katika maisha ya watu wa kawaida.
Janga la Black Death (Kifo Cheusi)
Idadi ya watu wa Norwe iliongezeka kutoka 150,000 hadi karibu 400,000 katika miaka kati ya 1000 na 1300AD, licha ya kuenea kwa vifo na magonjwa. Karibu nusu ya idadi ya watoto walifariki kabla ya kufikisha mwaka mmoja, na wanawake wengi walikufa wakati wa kujifungua.
Janga lilizuka katikati ya karne ya 14. Janga hili linajulikana kama Black Death kwa sababu walioambukizwa ugonjwa huo walipata vidonda vikubwa mwilini vilivyokuwa bluu-nyeusi. Wengi wa walioambukizwa walifariki baada ya siku chache tu. Inaaminika kuwa kati ya watu milioni 75 hadi 200 walifariki kote ulimwenguni kutokana na janga hilo. Karibu nusu ya walioishi Ulaya walifariki. Thuluthi moja ya watu nchini Norwe walifariki kutokana na ugonjwa huo.
Utawala wa kanisa, mfalme na wakuu
Watu wengi walikuwa wakulima wakati wa Zama za Kati. Katika Kipindi cha Maharamia, wakulima wengi walikuwa na mashamba na ardhi yao, lakini walihitajika kulipa ushuru kwa kanisa, mfalme na wakuu. Mtu yeyote aliyeshindwa kulipa ushuru huu ililazimika kusalimisha ardhi yake. Hii ilimaanisha kuwa kanisa, mfalme na wakuu waliendelea kutajirika nao watu wa kawaida walizidi kuwa maskini.
Miji ya kwanza nchini Norwe ilianzishwa katika kipindi hiki. Miji mikubwa ilikuwa Bergen (Bjørgvin), Trondheim (Nidaros), Oslo, Stavanger na Tønsberg.
Muungano
Ushawishi wa Denmaki kwa Norwe uliongezeka katika karne ya 14, na Norwe iliungana na Denmaki na Uswidi kuanzia 1397. Muungano huu ulikuwa na mfalme mmoja. Baadaye, Uswidi ulijiondoa, lakini muungano kati ya Denmaki na Norwe ulidumu hadi 1814. Muungano ulitawaliwa nchini Denmaki. Mji mkuu wa Denmaki, Copenhagen ulikuwa kituo cha kitamaduni cha muungano, na Wanorwe walisoma na kuandika Kidenmaki. Wakulima wa Norwe walilipa ushuru kwa mfalme huko Copenhagen, na Wanorwe walikwenda huko kusoma.
Uprotestanti
Uasi wa kidini ulianza mnamo 1517. Mtawa wa Ujerumani Martin Luther alipinga utawala wa Kanisa Katoliki. Watu zaidi walianza kumuunga mkono Martin Luther. Waliitwa waprotestanti kwa sababu waliasi. Wafalme kadhaa wa Ulaya Kaskazini pia walimuunga mkono Martin Luther. Mfalme wa Denmaki alibadilisha dini kwenda Uprotestanti. Uprotestanti ulikuwa dini rasmi nchini Norwe hadi mwaka wa 2012 ambapo mfumo wa kanisa rasmi ulikomeshwa.
Jadilianeni pamoja
- Je, kipindi hiki cha historia kilikuwaje katika nchi yako?
- Je, nchi yako iliathiriwa na janga la Black Death (Kifo Cheusi)?
- Je, hali hiyo inalingana kwa vyovyote vile na hali ya sasa?
- Dini ilikuwa muhimu sana katika maisha ya watu. Kanisa lilikuwa na ushawishi mkubwa. Je, unadhani hii iliwaathiri watu vipi? Hali ikoje leo?
- Je, unadhani muungano wa Norwe na Denmaki uliathiri vipi Wanorwe na maendeleo ya jamii?
Chagua jibu sahihi
Je, idadi gani ya Wanorwe walifariki kutokana na janga la Black Death (Kifo Cheusi)?
Chagua jibu sahihi
Je, Norwe iliungana na Uswidi na Denmaki mwaka gani?
Chagua jibu sahihi
Je, mtawa wa Ujerumani Martin Luther alipinga nini mwanzoni mwa karne ya 16?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?