Kuwalea watoto
Tazama filamu
Kuwalea watoto
Kuwalea watoto kunaweza kutofautiana katika familia, jamii na tamaduni mbalimbali. Wazazi wana jukumu kuu la kuwalea watoto wao, ingawa wao pia huiga mitindo ya ulezi ya watu wazima wengine katika chekechea, shuleni na kwenye shughuli za burudani. Lengo la kuwalea watoto, pamoja na mengine, ni kuwafundisha kushiriki katika jamii, kuwapa maadili mema ya kimsingi na kuwawezesha kuishi maisha mazuri.
Wazazi wanataka kutumia muda mwingi na watoto wao, na wanataka kujua mengi kuhusu kile watoto wao hufanya wakati hawako pamoja. Hivyo basi, ni muhimu kwa wazazi kudumisha ushirikiano mzuri kati yao na shule. Wazazi wengi pia wanachukulia kuwa ni muhimu kuwajua marafiki wa watoto wao pamoja na wazazi wao.
Mitazamo kuhusu jinsi watoto wanalelewa imebadilika. Watoto walichukuliwa kama ‘watu wazima wadogo’, na mara nyingi walihitajika kufanya kazi ili kuchangia mapato ya familia zao. Leo, maisha ya utotoni ni wakati wa kucheza na kujifunza, na watoto hawahitajiki kutekeleza majukumu kama hapo awali.
Watoto huleta furaha nyingi na ni jukumu kubwa, lakini wazazi wengi wakati mwingine huona kuwa kuwalea watoto ni kibarua kigumu. Watoto huwa hawatii wazazi wao kila wakati, na wakati mwingine wazazi huchoshwa, hukasirika na kufadhaika. Katika hali hizo, wanaweza kuzungumza na wazazi wengine, kusoma vitabu, kutafuta maelezo mtandaoni au kutafuta ushauri kutoka kwa watu wanaofahamu mengi kuhusu masuala hayo. Ni vyema kuwaza mapema kuhusu matatizo yanayoweza kutokea.
Jadilianeni pamoja
- Je, shule zinaweza kuwasaidia vipi wazazi kuhusiana na kulea watoto?
- Jadilianeni pamoja kuhusu mitazamo kuhusu watoto na jinsi ya kuwalea nchini Norwe.
- Jadilianeni pamoja kuhusu changamoto za kuwalea watoto.
Chagua jibu sahihi
Zamani, watoto walichukuliwa kuwa ‘watu wazima wadogo’. Je, watoto walihitajika kufanya nini zamani, ambayo hawapaswi kufanya sasa?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani ana jukumu kuu la kuwalea watoto?
Kamilisha sentensi
Ni furaha kubwa kupata watoto, na wazazi wengi wanachukulia...
Chagua jibu sahihi
Je, unaweza kufanya nini unapokabiliwa na changamoto kama mzazi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?