Wageni nchini Norwe

  • Je, kwa nini watu huhamia nchi zingine? Je, matarajio yao ni gani katika nchi mpya?
  • Je, ulijua nini kuhusu Norwe kabla ya kuja hapa? Ulipata habari hiyo wapi? Je, habari hiyo ilikuwa sahihi?
  • Ukilinganisha Norwe na nchi uliyotoka, zinafanana zaidi kwa njia zipi? Je, zinatofautiana zaidi kwa njia zipi?
  • Je, unadhani maisha ya kawaida yakoje nchini Norwe?
  • Je, unafahamu nini kuhusu Wanorwe?

Watu huhamia maeneo na nchi mpya kila mara. Huenda sababu zao ni tofauti. Wengine huhama kwa sababu ya hali yao ya kifedha, kazi au mapenzi, wengine huhama kwa sababu ya vita. Watu wengine wanapenda kujivinjari na wanataka tu mazingira mapya, au wanataka kusoma katika chuo kikuu mahususi.

Kufikia mwaka wa 2024, Norwe ina takriban watu milioni 5.5. Zaidi ya milioni moja kati yao walizaliwa nchi zingine au wazazi wao wametoka nje ya nchi. Hiyo ni takriban asilimia 20 ya idadi ya watu wanaoishi Norwe. Karibu nusu ya wahamiaji nchini Norwe wana uraia wa Norwe.

Kwa viwango vya leo, watu nchini Norwe walikuwa maskini sana karibu miaka 100 iliyopita. Hata hivyo, japo watu walikuwa maskini, Norwe bado iliongoza ulimwenguni katika ukadiriaji wa muda wa kuishi. Norwe ni nchi tajiri hivi leo. Hali ya maisha inalingana na kiwango katika nchi zilizo bora zaidi ulimwenguni. Kila mtu anaishi maisha tofauti, lakini hata hivyo watu wanaoishi hapa wana sifa nyingi zinazolingana.

  • Watu wengi wana fedha za kutosha. Wanamiliki au wanakodisha nyumba yao, wana chakula cha kutosha na nguo, na hata wana pesa zilizobaki.
  • Serikali hutoa huduma na usaidizi kwa watu wanapowahitaji.

Chanzo: SSB (Ofisi ya Takwimu ya Norway)

Tips til undervisningen

På youtube ligger det små filmer/bildeserier som viser norsk natur.

Bruk gjerne boka til Julien S. Bourrelle “The Social Guidebook to Norway” som en humoristisk inngang til nordmenns liv og væremåte.

Snakk sammen

Stikkord til refleksjonsoppgavene: krig, politikk, framtidsutsikter, utdanning, kjærlighet, familie, eventyrlyst, økonomi, klima

Man kan sammenlikne familieliv, arbeidsmarked, utdanningsmuligheter, geografi, historie, natur, klima, religion, politikk

Hva visste deltakerne før de kom? Hva vet de nå? Har noen synspunkter/oppfatninger/tanker endret seg?

Snakk om kunstverket

Kjerre, kvinner med skaut og to menn som skal utvandre til Amerika. Maleri.
Foto: O. Væring Eftf. AS «Utvandrere» malt av Gustav Wentzel (1900).

Tips til undervisninga

På YouTube ligg det små filmar/biletseriar som viser norsk natur.

Bruk gjerne Julien S. Bourrelle si bok "The Social Guidebook to Norway" som ein humoristisk introduksjon til livet og veremåten til nordmenn.

Snakk saman

Stikkord til refleksjonsoppgåvene: krig, politikk, framtidsutsikter, utdanning, kjærleik, familie, eventyrlyst, økonomi, klima

Ein kan samanlikne familieliv, arbeidsmarknad, utdanningsmoglegheiter, geografi, historie, natur, klima, religion, politikk

Kva visste deltakarane før dei kom? Kva veit dei no? Har dei endra synspunkt på eller meiningar/tankar om noko?

Snakk om kunstverket

Kjerre, kvinner med skaut og to menn som skal utvandre til Amerika. Maleri.
Foto: O. Væring Eftf. AS «Utvandrere» malt av Gustav Wentzel (1900).