Mpango wa kuwakaribisha wageni na Sheria ya Ushirikishaji
Mpango wa kuwakaribisha wageni na Sheria ya Ushirikishaji
Lengo la mpango wa kuwakaribisha wageni ni:
- kuwapa wageni ujuzi wa msingi wa lugha ya Kinorwe
- kuwapa wageni maelezo ya kimsingi kuhusu jamii ya Wanorwe
- kuwandaa wageni kwa ajili ya ajira au elimu
Wakuu wa serikali nchini Norwe wanatambua kuwa ni vigumu kwa watu kupata kazi na kujitegemeza wanapofika katika nchi mpya. Hivyo basi, Bunge la Norway (Storting), lilipitisha sheria inayojulikana kama Sheria ya Ushirikishaji. Miongoni mwa mambo mengine, sheria hii inazipa manispaa za Norwe jukumu la kuendesha mpango wa kuwakaribisha wakimbizi.
Katika mpango huu, wageni hujifunza Kinorwe na kupata maarifa na mafunzo kuhusu Wanorwe na hali ya ajira nchini Norwe. Lengo la mpango huu ni kwa washiriki kupata ajira au elimu wanapomaliza mpango. Mpango huu huchukua kati ya miezi mitatu na miaka mitatu, kulingana na kiwango cha masomo na uzoefu wa mtu husika. Wanaoshiriki katika mpango hupokea msaada wa kifedha.
Utangulizi wa mpango unajumuisha:
- Kujifunza Kinorwe
- kupata usaidizi kuhusu kuzoea maisha katika nchi mpya
- mwongozo wa wazazi (kwa wale walio na watoto chini ya umri wa miaka 18)
- maudhui yanayohusiana na kazi au elimu
Chanzo: IMDi
Jadilianeni pamoja
- Je, kwa nini wakimbizi wanashirikishwa katika mipango ya kuwakaribisha?
- Je, kwa nini wahamiaji wote hawashirikishwi katika mipango ya kuwakaribisha?
- Je, masharti yapi yanapaswa kuwekewa wanaoshiriki katika mpango wa kuwakaribisha wageni?
- Je, unadhani wanaoshiriki katika mpango wanatarajia nini? Je, jamii inatarajia nini kutoka kwa wanaoshiriki katika mpango huu?
Chagua jibu sahihi
Je, lengo la mpango wa kuwakaribisha wageni ni gani?
Chagua jibu sahihi
Je, mpango wa kuwakaribisha wageni huchukua muda gani?
Chagua jibu sahihi
Je, Sheria ya Ushirikishaji ilipitishwa na nani?
Chagua jibu sahihi
Je, mpango wa kuwakaribisha wageni hutolewa na nani?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?