Fedha za kibinafsi
Fedha za kibinafsi
Mapato ni pesa zote zinazoingia kwenye akaunti yako ya benki (mshahara, malipo ya usalama wa kijamii au fedha zingine kutoka NAV, mafao ya watoto, "msaada wa kifedha" kwa wazazi, nk.).
Matumizi ni kila kitu tunachogharamia kifedha (kodi, riba na malipo ya polepole, chakula, mavazi, usafiri, umeme, intaneti, shughuli za starehe nk.).
Malipo ya jumla: Mapato/mshahara kabla ya kutozwa ushuru
Malipo halisi: Mapato/mshahara baada ya kutozwa ushuru
Mapato na matumizi
Gharama ya maisha iko juu nchini Norwe. Wazazi wote katika familia nyingi wanafanya ajira mbali na nyumbani. Katika familia zingine, mama na/au baba anaweza kufanya kazi kwa saa chache watoto wakiwa wadogo (kazi kwa muda), nao watu wengi wanahitaji kazi ya kudumu ili waweze kujikimu. Watu wazima wote katika familia wanawajibikia fedha za familia.
Watu wazima wengi hupokea malipo, usalama wa kijamii au pensheni mara moja kwa mwezi nchini Norwe. Iwapo kuna mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 katika familia, watapokea pia mafao ya watoto. Wazazi hupokea "msaada kamili wa kifedha" kwa watoto wadogo ambao hawaendi chekechea.
Mafao ya watoto: Msaada wa kifedha unaotolewa kwa ajili ya watoto wote walio chini ya umri wa miaka 18 nchini Norwe. Umekusudiwa kusaidia kulipia gharama zinazotokana na mtoto.
"Msaada wa kifedha" kwa wazazi: Msaada wa kifedha unaotolewa kwa ajili ya watoto wote walio kati ya mwaka mmoja na miaka miwili ambao hawahudhurii chekechea. Fedha zinazotolewa hupunguzwa kwa watoto walio chekechea.
Unaweza kupata maelezo kuhusu mafao ya watoto na "msaada wa kifedha" kwa wazazi kupitia tovuti ya NAV.
Akaunti ya benki
Watu wazima wote nchini Norwe wana akaunti binafsi za benki. Watoto wengi na vijana pia wana akaunti. Unapopokea mshahara, malipo ya usalama wa kijamii au pensheni, pesa huenda moja kwa moja kwenye akaunti yako ya benki. Ili ufungue akaunti ya benki, unahitaji nambari ya kitambulisho cha kibinafsi cha Norwe au nambari ya kitambulisho cha muda cha Norwe.
Benki ya mtandaoni
Watu wazima hutumia benki ya mtandaoni. Hii inafanya iwe rahisi kudumisha muhtasari wa akaunti yako ya benki, kufuatilia mapato na matumizi na kulipa bili. Unaweza kufikia benki mtandaoni ukitumia kompyuta, kompyuta kibao au simu mahiri. Ili uweze kuingia, unahitaji BankID (kitambulisho cha benki) au kizalishaji cha msimbo wa benki.
Mikopo ya benki
Nchini Norwe, ni kawaida kukopa benki pesa ili kununua vitu vikubwa kama vile nyumba au gari. Unapokopa pesa, unafanya makubaliano na benki. Upo mpango wa malipo unaoonyesha kiasi ambacho mtu anahitajika kulipa kila mwezi au robo ya mwaka. Riba na malipo ya polepole yanalipwa kwa benki.
Malipo ya polepole: Pesa za kulipia mkopo, yaani unacholipa kwa kuchukua mkopo.
Riba: Tunalipa riba kwenye benki. Riba ni gharama ya kukopa pesa. Riba ni asilimia fulani ya mkopo wako.
Kawaida, riba na malipo ya polepole hulipwa kila mwezi au kila robo ya mwaka.
Bajeti
Hati inayoonyesha mapato na matumizi kwa kipindi mahususi. Bajeti huundwa na kampuni na watu binafsi. Familia nyingi huandaa bajeti kila mwezi. Hii inafanya iwe rahisi kudumisha muhtasari wa mapato na matumizi. Kisha familia zinaweza kupanga jinsi watakavyotumia pesa zao. Bajeti inapaswa kujumuisha pesa zinazoweza kutengwa kila mwezi kwa madhumuni ya kuweka akiba au matumizi yasiyotarajiwa.
Jadilianeni pamoja
- Je, familia ya kawaida nchini Norwe ina mapato na gharama zipi?
- Je, gharama zipi zisizotarajiwa huenda zikatokea?
- Je, wewe hutumia pesa nyingi kufanya nini?
- Je, unaweza kufanyaje kupunguza matumizi yako ya pesa?
Berg na familia yake wameketi sebuleni. Mama na baba wameandaa bajeti ya mapato na matumizi kwa mwezi. Baada ya kugharamikia matumizi yote muhimu, wamebaki na karibu NOK 4,000. Sasa wanazungumzia kuhusu watakachotumia pesa hizi kufanya.
- Mama angependa koti mpya ya kuvalia msimu wa baridi. Aliyonayo ni ya zamani na ni nzee.
- Baba angependa kuweka akiba. Je, gharama zisizotarajiwa huenda zikatokea?
- Mwanawe angependa kwenda kufanya mazoezi ya soka na marafiki zake. Anahitaji pia viatu vipya vya kuchezea kandanda.
- Bintiye anahitaji begi mpya ya shule. Amekua mkubwa pia na anahitaji nguo mpya.
Jadilianeni pamoja kuhusu jinsi familia inapaswa kutanguliza matumizi ya pesa.
Chagua jibu sahihi
Je, mapato ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, mshahara/mapato ya jumla ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, bajeti ni nini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?