Kutafuta kazi
Tazama filamu
Kutafuta kazi
Ombi la kazi na wasifu kazi
Japo ukosefu wa ajira uko chini nchini Norwe, bado kunaweza kuwa na ushindani mkubwa kwa nafasi za kazi zilizopo. Ikiwa ungependa kupata kazi, sharti utafute. Ni muhimu kushirikisha watu unaowasiliana nao na unaowajua na kuonyesha kuwa una haja ya kufanya kazi. Unapopata kazi ambayo ungependa, huenda ukahitaji kuwasilisha ombi na wasifu kazi.
Ombi la kazi ni barua unayoandika ili kujitambulisha na kuelezea kuhusu historia yako. Wasifu kazi ni hati unayoandika ili kuelezea kwa ufupi kuhusu elimu na uzoefu wako wa kazi. Unapaswa kuandika ombi la kazi na wasifu kazi kwa Kinorwe sahihi. Maelezo yote unayotoa sharti yawe sahihi. Ni muhimu kuandika hati hizo kwa njia sahili.
Mwajiri anayehitaji mfanyakazi mpya ataangazia anayefaa zaidi kwa nafasi hiyo ya kazi. Atazingatia ikiwa aliyetuma ombi ana elimu inayofaa au anastahiki, lakini vitu vingine pia ni muhimu.
Je, atakayeajiriwa ana
- uzoefu
- wadhamini wa kuaminika
- sifa inayoendana na mazingira ya kazini
- sifa zinazostahili kwa nafasi hiyo
Mahojiano
Kabla ya mwajiri kuamua ni nani atakayepata kazi, kwa kawaida atawahoji mara moja au zaidi waliotuma maombi ya kazi. Kwenye mahojiano, aliyetuma ombi la kazi ana fursa ya kujiwasilisha mwenyewe na anayehusika na kuajiri ataweza kumfahamu. Wote wanaweza kuuliza maswali.
Vidokezo kuhusu mahojiano:
- Fahamu mahojiano yatafanyika wapi na jinsi ya kufika hapo.
- Fikiria kuhusu mavazi yako na jinsi ungependa kuonekana.
- Fika kwa wakati.
- Kusalimiana kwa ujasiri na kuangaliana kwa macho ni muhimu.
- Kuwa mchangamfu, tabasamu na jaribu kujenga uhusiano kati yako na wanaokuhoji.
Jadilianeni pamoja
- Je, kuandika barua ya maombi ya kazi ni muhimu katika nchi yako?
- Elezea unachopaswa kujumuisha unapoandika barua ya ombi la kazi.
- Je, ni mambo gani unayopaswa kuuliza wakati wa mahojiano, na ni yepi unayopaswa kuepuka?
- Fafanua unachopaswa kuvalia unapokwenda kwenye mahojiano.
Chagua jibu sahihi
Je, ombi la kazi ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, wasifu kazi ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani anayeweza kuuliza maswali kwenye mahojiano ya kazi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?