Elimu ya watu wazima
Elimu ya watu wazima
Jamii inabadilika kila wakati. Teknolojia mpya imeathiri hali ya ajira. Wafanyakazi wanapaswa kuendelea kujikuza na kujifunza ujuzi mpya. Watu wazima wanaweza kusoma upya, kuendeleza masomo yao ya awali au kufanya masomo ya shule ya msingi au ya kati ili kukidhi mahitaji mapya kazini. Watu wazima wengi pia wanaendelea na masomo ya baada ya sekondari na masomo zaidi huku wakiendelea na kazi zao. Tunazidi kujifunza maishani na hii inajulikana kama masomo bila kikomo.
Elimu ya maandalizi na sekondari kwa watu wazima
Watu wazima wana haki ya kupokea elimu ya maandalizi kwa watu wazima (FOV) ikiwa hawajamaliza elimu ya msingi hapo awali. Elimu ya maandalizi kwa watu wazima haina malipo. Munispaa inawajibika kutoa elimu hii.
Watu wazima waliofikisha umri wa miaka 25 wana haki ya kupata elimu ya upili ikiwa hawajafika hapo. Unahitaji kuwa umekamilisha masomo ya shule ya msingi na ya kati nchini Norwe au katika nchi nyingine kabla ya kuanza masomo ya upili. Mamlaka za kaunti zinawajibikia elimu. Elimu ya upili kwa watu wazima hailipishwi katika shule za umma. Shule nyingi za kibinafsi zinapatikana pia. Shule hizi zinalipisha karo.
Japo hakuna kulipa karo, watu wazima wanahitaji pesa kukithi mahitaji ya kila siku. Hivyo wengi wao wanaweza kupata udhamini na/au kukopa pesa kutoka kwenye Mkopo wa Serikali wa Kufadhili Elimu wakiendelea na masomo.
Elimu yako hutambuliwa japo umesomea nchi nyingine
Ikiwa umefuzu kutoka nchi zingine, unaweza kuwasilisha ombi ili masomo yako yatambuliwe nchini Norwe. Ombi hili huwasilishwa kupitia HK-dir. Wahudumu wa afya wanaweza kuomba idhini kutoka kwa Mamlaka ya Afya.
Ongea na mshauri katika shule yako au mshauri wa wakimbizi ili upate maelezo zaidi kuhusu chaguo zako.
Tathmini ya uwezo
Tunaweza kupata ujuzi kupitia elimu na kupitia uzoefu mwingine. Huenda ikawa ngumu kwa wanaokuja Norwe wakiwa watu wazima kuthibitisha uwezo wao kwa kuwasilisha vyeti. Badala yake, ujuzi na uzoefu wao wa awali wa kazi unaweza kutathminiwa. Hii inamaanisha kuwa ujuzi wa mtu binafsi hutathminiwa kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa. Tathmini inaweza kusababisha mtu kuruhusiwa kufanya kozi kwa muda mfupi, kusajiliwa kufanya kozi fulani, kutojumuishwa katika masomo fulani, kupata kazi mpya au nyongeza ya mshahara. Tathmini inawezekana katika kiwango cha shule ya msingi na ya kati, kuhusiana na elimu ya kiufundi na katika kiwango cha elimu ya juu.
Jadilianeni pamoja
- Je, mtazamo wako ni upi kuhusu suala la masomo bila kikomo?
- Jadilianeni kuhusu jinsi maendeleo ya kijamii yanaathiri hitaji la mtu binafsi la maarifa na ujuzi mpya.
Chagua jibu sahihi
Je, watu wazima wanaweza kupata lini elimu ya bila malipo katika shule ya msingi na ya kati?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani anayewajibikia elimu ya shule ya msingi na ya kati, kwa watu wazima?
Chagua jibu sahihi
Watu wazima ambao wamefikisha umri wa miaka 25 wana haki ya kupata elimu ya shule ya kati ikiwa hawajafikia kiwango hicho. Je, unahitaji kuwa umefikia kiwango gani cha masomo ili kupata haki hii?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?