Utambulisho
Tazama filamu
Utambulisho
Jinsi tunavyojitambua hujulikana kama utambulisho. Utambulisho huundwa kutokana na tabia na sifa zetu. Vigezo vya kijamii kama vile unakoishi, unaotangamana nao na mambo yanayotuvutia pia huchangia katika utambulisho.
Utambulisho wa kijinsia
Unayempenda na kuvutiwa naye kimapenzi husaidia kubainisha mwelekeo wetu wa kimapenzi. Watu wengine hujitambulisha kuwa mashoga, wengine huvutiwa na jinsia ya pili nao wengine hawabainishi mwelekeo wao wa kimapenzi.
Utambulisho wa kijinsia
Jinsia ni sehemu ya utambulisho wetu. Kawaida, fiziolojia hutumika kubaini jinsia zetu tunapozaliwa kama mvulana au msichana. Hii imeimarishwa na mifumo dhahiri ya majukumu ya kijinsia. Leo, uainishaji huu unachukuliwa kuwa finyu kwa kutowajumuisha watu wote, na wapo watu wanaotaka kujitambulisha kuwa wa jinsia nyingine kando na hizi mbili, au jinsia zao ziko kati ya jinsia hizi mbili za kawaida. Utambulisho wa kijinsia ni neno linalotumika kufafanua jinsi watu wanavyovaa au kusisitiza jinsia zao.
Jadilianeni pamoja
- Jadili uhusiano uliopo kati ya utambulisho na utofauti.
- Je, kuna ufinyu upi katika kuainisha jinsia katika vikundi viwili? Je, inasaidia vipi?
- Je, unahusisha nini na kauli 'utambulisho wa kijinsia'?
- Je, unadhani changamoto ni zipi kwa mtu anayejitambulisha vinginevyo kijinsia au kimapenzi?
- «LGBTQI+» mara nyingi hutumiwa kuhusu watu wanaovunja kanuni za jinsia na ujinsia Jua kile herufi zinawakilisha.
Kamilisha sentensi
Utambulisho wetu hutokana na tabia zetu na...
Kamilisha sentensi
Unayempenda na kuvutiwa naye kimapenzi husaidia kubainisha...
Kamilisha sentensi
Jinsi watu wanavyovaa au kusisitiza jinsia zao kwa njia zingine, inajulikana kama...
Chagua jibu sahihi
Je, ni nini huimarisha jinsia yetu ya kifiziolojia?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?