Wasami
Wasami
Wasami ndio wenyeji asilia wa Norwe. Wasami wanaishi katika nchi nne: Norwe, Uswidi, Ufini na Urusi. Wasami ndio kikundi kongwe zaidi cha watu nchini Norwe, na kuna lugha kadhaa za Wasami. Lugha za Kisami ni tofauti kabisa na Kinorwe. Mtu anayezungumza Kinorwe pekee hawezi kuelewa Kisami. Karibu Wasami wote wa Norwe leo wanafahamu Kinorwe. Wengi pia huzungumza lugha ya Kisami.
Siku ya Kitaifa ya Wasami huadhimishwa tarehe 6 Februari. Siku hiyo, bendera ya Wasami hupeperushwa Norwe siku nzima. Wasami wana sare za kitaifa zinazojulikana kama "kofte". Wasami bado huvalia vazi hili wakati wa hafla maalum kama vile harusi. Baadhi ya Wasami huvalia vazi hili kila siku.
Wanorwe walijaribu kuwasimilisha Wasami karibu miaka 150 iliyopita. Watoto wa Wasami walihitajika kusomea shule za Wanorwe, na hawakuruhusiwa kujifunza Kisami. Mnamo 1959, lugha ya Kisami iliruhusiwa tena kutumika shuleni. Mnamo 1902, sheria ilibuniwa na kubainisha kuwa ili mtu aruhusiwe kununua kipande cha ardhi, sharti awe raia wa Norwe anayeweza kuzungumza, kusoma na kuandika Kinorwe. Sheria hii ilitekelezwa hadi mnamo 1965. Hali ni tofauti sana hivi leo. Bunge la Wasami, Sametinget, lilifunguliwa mnamo 1989. Jukumu la Bunge la Wasami ni kulinda haki za Wasami nchini Norwe, haswa kuhusiana na utamaduni na elimu. Wajumbe wa Bunge la Wasami huchaguliwa baada ya kila miaka minne.
Jadilianeni pamoja
- Je, kuna makundi ya wenyeji asilia katika nchi yako? Je, maisha yao yako vipi?
- Jadili kuhusu hali za makundi mbalimbali ya walio wachache.
Chagua jibu sahihi
Je, Wasami wanaishi katika nchi zipi?
Chagua jibu sahihi
Je, tangu jadi Wasami wamejikimu vipi kimaisha?
Chagua jibu sahihi
Mnamo 1902, sheria ilibuniwa na kubainisha kuwa ili mtu aruhusiwe kununua kipande cha ardhi, sharti awe anaweza kuzungumza, kusoma na kuandika Kinorwe. Je, sheria hii ilibatilishwa lini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?