Mitandao ya kijamii na kuchuja maneno mtandaoni
Tazama filamu
Mitandao ya kijamii na kuchuja maneno mtandaoni
Leo, watu wengi hutumia sana Intaneti na mitandao ya kijamii. Tunaingia kwenye benki zetu za mtandaoni au tunatembelea huduma za umma mtandaoni, na tunanunua mtandaoni. Tunajitambulisha kwa kutumia BankID (kifaa cha uthibitishaji), nenosiri, alama za vidole au utambuzi wa uso.
Mitandao ya kijamii inahusisha Facebook, Twitter na Instagram. Tunashiriki maoni, picha na video zetu kwenye mitandao hii. Inatuwezesha kuwasiliana na familia, marafiki na watu tunaowafahamu. Tunapotumia huduma hizi tunashiriki maelezo mengi ya kibinafsi, na maelezo haya yote huhifadhiwa. Je, umefikiria kuhusu kinachoweza kutokea maelezo hayo ya kibinafsi yakifikiwa na mtu mwenye nia mbaya? Je, kipi kitatokea mtu mwingine akipata nenosiri yako? Je, mtu mwingine akishiriki picha zako binafsi?
Ni muhimu kufahamu unachoshiriki, unayeshiriki maelezo naye, na jinsi maelezo hayo yatakavyotumiwa. Kwa mfano, picha binafsi, kama vile picha za watoto, zinaweza ‘kuibiwa’ na mtu ambaye atazitumia vibaya. Lazima pia tuwe waangalifu kuhusu tunachoshiriki kuhusu watu wengine. Omba ruhusa kwanza kila wakati.
- Ulinzi wa data unahusu haki ya faragha na kudhibiti data yako ya kibinafsi. Maelezo ya kibinafsi ni, kwa mfano, jina, anwani, nambari ya simu, nambari ya kitambulisho cha kitaifa na asili ya kikabila.
- Kila mtu ni wa maana. Hivyo basi watu wana haki ya kufanya mambo yao binafsi na kuwa mahali ambapo wanaweza kutekeleza shughuli jinsi wapendavyo bila kushurutishwa au kukatizwa na serikali au watu wengine. Kanuni hii ipo, pamoja na sheria zingine, katika Mkataba wa Ulaya kuhusu Haki za Binadamu (ECHR).
Chanzo: Mamlaka ya ulinzi wa data nchini Norwe
Watu wengi hushiriki maoni yao kwenye mitandao ya kijamii na mtandaoni kwa jumla. Watu huandika, hujadili na kuzungumzia masuala. Haki ya kujieleza inatumika sana kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, haki ya kujieleza imewekewa vikwazo kwa mujibu wa sheria za ulinzi wa data na vifungu kadhaa vya kisheria. Watu hawaruhusiwi kuandika kauli zinazoonyesha ubaguzi. Wengine hukiuka sheria hizi hata hivyo. Watu hukiuka kanuni hizi kwa urahisi zaidi mtandaoni kuliko wanapozungumza na mtu ana kwa ana. Maoni mengi ya kukera na yasiyoruhusiwa hutolewa haswa wakati anayeandika hajulikani. Hatua mwafaka ya kuchuja unachoshiriki ni kuandika maoni mtandaoni ukitumia maneno unayoweza kumwambia mtu ana kwa ana pia.
Jadilianeni pamoja
- Je, matokeo yepi huonyeshwa unapotafuta jina lako mtandaoni?
- Jadili maana ya kuchuja unachoshiriki mtandaoni.
- Jadiliana kuhusu uhusiano uliopo kati ya ulinzi wa data na kuchuja unachoshiriki mtandaoni.
- Zungumzia umuhimu wa kujua unachochapisha kwenye mitandao ya kijamii.
- Je, unadhani matokeo ya watu kuandika maoni bila kujulikana ni gani?
Chagua jibu sahihi
Je, unapaswa kumwomba mtu ruhusa ya kushiriki picha zake kwenye mitandao ya kijamii?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nini hupaswi kuandika mtandaoni?
Chagua jibu sahihi
Je, kipi kinabainisha kuchuja unachoshiriki mtandaoni?
Chagua jibu sahihi
Je, ulinzi wa data unahusu nini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?