Kazi ya hiari (dugnad)
Tazama filamu
Kazi ya hiari (dugnad)
"Dugnad" ni kazi ya kujitolea isiyo na malipo. "Dugnad" ni kazi inayohusisha juhudi za jamii. Ni aina ya kawaida ya kazi katika makundi na mashirika. Kwa mfano, katika shirika linalohusikana na makaazi, wakaaji mara nyingi hushiriki kwenye "dugnad" katika msimu wa machipuko ili makaazi yao yawe nadhifu baada ya msimu wa baridi. Ni kawaida katika shule nyingi za chekechea kwa wazazi kushirikiana pamoja katika "dugnad" mara moja au mara kadhaa kwa mwaka. Wanaweza kusafisha vitu vya watoto vya kuchezea au kukarabati maeneo ya nje shuleni.
Watoto wengi nchini Norwe hushiriki katika shughuli za burudani zilizopangwa, na nyingi yazo huendeshwa na wazazi kupitia dugnad. Kwa mfano, wazazi wanaweza kuandaa mauzo au hafla ya kitamaduni ili kukusanya pesa za kufadhili shirika.
"Dugnad" ni desturi ya zamani nchini Norwe. Jamii nyingi za wakulima ulimwenguni zina desturi kama hii.
Mwaka wa 2004, neno ‘dugnad’ lilifanywa kuwa neno la kitaifa nchini Norwe.
Jadilianeni pamoja
- Je, maoni yako ni yepi kuhusu "dugnad"? Je, tayari unafahamu kuhusu hili?
- Je, umewahi kualikwa kushiriki katika shughuli ya hiari (dugnad) nchini Norwe?
- Baadhi ya makundi na mashirika yana chaguo la kulipa kiasi fulani ili usishiriki kwenye "dugnad". Je, unachukulia vipi hilo?
Ni Jumatatu. Baba wawili wako kwenye shule ya chekechea kuchukua watoto wao. Wanazungumza kuhusu "dugnad" iliyofanyika wikendi iliyopita katika shule ya chekechea.
Henrik: Ninafurahi kukuona tena! Ilikuwa ya kusisimua kuona kazi tuliyofanya! Chumba kipya cha watoto kuchezea sasa ni kizuri sana!
Arne: Naam. Ni vyema kushirikiana hivyo pia. Lakini wazazi wa Truls hawajawahi kushiriki kwenye "dugnad".
Henrik: Nimegundua pia. Japo "dugnad" ni jambo la hiari, si vyema kukosa.
Arne: Naam. Nimegundua wakati mwingine huenda shughuli inayofanywa haikufai, lakini kukosa kila wakati ni vizuri kweli...?
Henrik: Aisee… na nina uhakika Truls angependa kutumia chumba cha kuchezea kama watoto wengine.
- Jadili hali inayozungumziwa hapa juu. Je, kwa nini Henrik na Arne wanachukulia mambo hivyo?
- Je, unadhani kipi kinaweza kutokea mtu anapokosa kujitokeza kwa ajili ya "dugnad"?
Chagua jibu sahihi
Je, "dugnad" ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, kawaida watu hufanya kazi zipi za kujitolea katika shule za chekechea?
Chagua jibu sahihi
Je, kawaida nani huandaa "dugnad"?
Chagua jibu sahihi
Je, kazi za hiari zipo Norwe pekee?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua picha sahihi
Je, picha zipi zinaonyesha shughuli za kawaida za "dugnad"? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.