Kuhamia nchi nyingine
Kuhamia nchi nyingine
Sebene: Ninafuraha sana kuwa hatimaye tumefika Norwe. Nchi hii ni nzuri sana, na ninahisi kwamba siku za usoni ni salama sasa, kwetu na kwa watoto wetu.
Amaniel: Huku ni kuzuri? Nimechoka kuwa katika nchi ya kigeni. Mambo ni magumu sana. Hakuna kinachofanya kazi. Sina kazi, sielewi lugha na ninahitaji usaidizi kwa kila kitu. Wenyeji wana tabia za kushangaza sana. Mtazamo wao wa maisha ni tofauti kabisa.
Sebene: Nilidhani mambo yalikuwa shwari.
Amaniel: Mambo yalikuwa mazuri wiki chache zilizopita. Sikufahamu jinsi maisha yalikuwa yamebadilika. Tumepoteza mengi: familia, marafiki, mila na lugha yetu.
Watu wanaohamia nchi nyingine hupitia mchakato fulani. Mara nyingi hupitia mchakato unaojulikana kama uhamaji wa kiakili wa awamu tatu. Kila mtu ana muda tofauti wa kukamilisha kila awamu.
Awamu ya 1
Mwanzoni, ni kawaida kuhisi mwenye furaha na matumaini. Kawaida, shughuli huwa nyingi. Kuna mengi ya kushughulikia, na inasisimua kwamba kila kitu ni kipya kwako. Watu huwaza zaidi kuhusu fursa mpya ambazo wamepata, na kutofikiria sana kuhusu walichoacha nyuma na kupoteza.
Awamu ya 2
Baada ya siku, wiki au miezi michache, watu wengi huhisi maisha ni magumu katika nchi mpya. Wanagutuka na kufahamu athari za kuhamia nchi nyingine. Kila kitu wasichofahamu katika nchi hiyo mpya kinaweza kuwafanya wasijihisi salama. Watu wanachoshwa na kukata tamaa kwa kuwa mambo ni tofauti, na wanaanza kutamani maisha waliyozoea.
Awamu ya 3
Baada ya muda, maisha huwa rahisi tena kwa watu wengi. Wanafahamu mengi zaidi, kuhusiana na lugha na mfumo katika nchi waliyohamia. Matumaini yapo kwa siku za usoni. Wamekubali kuwa wamehama. Hatua kwa hatua, wanaanza kutambua mazuri kuhusu maisha na maadili katika nchi mpya. Wanapokubali mambo yalivyo na wanapotumia uzoefu kutoka nchi yao, wanaweza kunawiri katika nchi hii mpya.
Jadilianeni pamoja
- Je, Amaniel na Sebene wako vipi? Je, hali yako inahusiana vipi na wanachosema?
- Amaniel anasema amepoteza mengi. Je, hii inaweza kuathiri vipi afya yake?
- Je, awamu hizo ni tofauti kati ya mtu ambaye amehamia nchi mpya bila hiari na yule amehama kwa hiari?
- Je, maisha yatakuwaje katika familia ikiwa wanafamilia wako katika awamu tofauti wakati tofauti?
Chagua jibu sahihi
Je, mchakato wa uhamaji wa kiakili una awamu ngapi?
Chagua jibu sahihi
Je, awamu ipi inahusisha...
- kuhisi maisha ni magumu katika nchi mpya
- kufahamu athari za kuhamia nchi nyingine.
- kutamani maisha uliyozoea
Chagua jibu sahihi
Je, awamu tofauti huchukua muda gani?
Kamilisha sentensi
Unapoanza kutambua mazuri kuhusu maisha na maadili katika nchi mpya kisha unatumia uzoefu kutoka nchi yao...
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?