Kuishi katika tamaduni mbili
Kuishi katika tamaduni mbili
Kila mtu huzaliwa katika jamii na utamaduni fulani. Katika utamaduni huu, tunajifunza jinsi ya kuishi pamoja, tofauti kati ya mema na mabaya, na jinsi tunavyoona nafasi yetu katika ulimwengu. Watoto hujifunza kutoka kwa wazazi wao na kupitia jamii inayowazunguka. Tamaduni tofauti zina misimamo tofauti kuhusu jukumu la mtu. Ili kuelewa tofauti hizi kwa urahisi, tunaweza kugawanya tamaduni katika makundi mawili makuu. Tunayaita makundi haya mawili tamaduni za kibinafsi na zilizo jumuishi.
Katika utamaduni wa kibinafsi, mtu ndiye muhimu zaidi. Maadili mema ni pamoja na uhuru na usawa. Katika utamaduni jumuishi, kikundi kwa ujumla ndiyo muhimu zaidi. Maadili mema ni pamoja na utiifu, heshima na uhusiano mzuri.
Kwa watoto wanaokuzwa katika tamaduni mbili, huenda wakati mwingine wakahitaji kuzingatia kanuni fulani wakiwa nyumbani na kanuni nyingine tofauti wakiwa kwingineko. Huenda kukawa na maoni tofauti kuhusu adabu au kinachochukuliwa kuwa sahihi, na kunaweza kuwa na matarajio tofauti kuhusu tabia ya mtoto.
Jadilianeni pamoja
- Jadili tofauti kati ya tamaduni za kibinafsi na zilizo jumuishi. Je, zinatofautiana kabisa moja kwa nyingine?
- Je, utamaduni wa Kinorwe ni utamaduni jumuishi, utamaduni wa kibinafsi au utamaduni wa mseto?
- Je, ni matatizo yapi humkabili mtu kutoka kwenye utamaduni jumuishi ikilinganishwa na utamaduni wa kibinafsi?
- Je, ni matatizo yapi humkabili mtu kutoka kwenye utamaduni wa kibinafsi kuhusiana na utamaduni jumuishi?
- Jadili kuhusu kuwalea watoto katika utamaduni wa kibinafsi na utamaduni jumuishi.
Chagua jibu sahihi
Je, watoto hujifunza kutoka kwa nani?
Chagua jibu sahihi
Ili kuelewa tofauti hizi kwa urahisi, tunaweza kugawanya tamaduni katika makundi mawili makuu. Je, makundi haya mawili yanaitwaje?
Chagua jibu sahihi
Je, tamaduni jumuishi zina sifa zipi?
Chagua jibu sahihi
Je, tamaduni za kibinafsi zina sifa zipi? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?