Afya ya kiakili
Afya ya kiakili
John: Bado nina maumivu ya tumbo. Silali vizuri.
Daktari: Tumekufanyia vipimo vyote, na hatujapata chochote kibaya kinachodhuru tumbo lako.
John: Sielewi.
Daktari: Unajihisi vipi? Je, bado unahisi huzuni na upweke?
John: Kwa nini unauliza? Tumbo langu ndilo lina tatizo.
- Kwa nini daktari anamuuliza John ikiwa anahisi huzuni na upweke?
- Je, kwa nini John ameghadhabishwa?
- Jadili uhusiano uliopo kati ya afya ya kiakili na kimwili.
- Je, suala la matatizo ya afya ya kiakili linachukuliwa vipi katika nchi yako na nchini Norwe?
- Je, ni nani anaweza kumsaidia John?
Wiki chache baadaye:
Daktari: Hujambo John! Nimefurahi kukuona tena. Nikusaidiaje?
John: Nimekuwa nikiwaza kuhusu tulichozungumza nilipokuwa hapa mara ya mwisho. Ninaona ninahitaji usaidizi. Ninahisi maisha ni magumu na yanachosha. Sina furaha na siku zote nimechoka. Wakati mwingine mimi hukasirika bila sababu. Silali vizuri na ninaota ndoto mbaya kuhusu mambo niliyopitia nilipokuwa katika nchi yangu.
Daktari: Nitakuelekeza kwa mwanasaikolojia.
John: Mwanasaikolojia? Sina matatizo ya kiakili.
Daktari: Huna, lakini kuzungumza na mtaalamu kuhusu matatizo yako kunaweza kusaidia. Kumbuka kuwa wanasaikolojia wana wajibu wa usiri na hawawezi kushiriki na mtu mwingine yeyote chochote ulichosema. Unaweza kwenda kumwona mara moja ili uone ikiwa utasaidika.
John: Kwenda kwangu hakutanidhuru zaidi. Nitajaribu.
- Je, unachukulia vipi mapendekezo ya daktari?
- Je, unachukulia vipi hulka ya John?
Watu wengi wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiakili maishani. Kuna sababu nyingi zinazopelekea watu kupata matatizo ya kiakili. Wakati mwingine, ni kutokana na hali ngumu ya maisha kama vile matatizo ya kifamilia au hali ngumu kazini. Watu wengine hupata matatizo ya kiakili baada ya shida, kifo, ajali au kutokana na matukio ya vita. Watu wengine huenda wakarithi matatizo ya kiakili, na mafadhaiko yanaweza kuwa kichochezi.
Unahitaji kuzungumza na mtu unapokabiliwa na shida. Unaweza kupata usaidizi kwa kuzungumza na familia au marafiki. Wakati mwingine, huenda ukahitaji usaidizi wa mtaalamu. Mwanasaikolojia au mtaalamu mwingine anaweza kukusaidia kupata suluhu la tatizo lako. Daktari wa kawaida anaweza kukuelekeza kwa mwanasaikolojia ikiwa unahitaji.
Mtazamo wa jamii kuhusu afya ya kiakili umebadilika. Leo, idadi kubwa ya Wanorwe wana mtazamo pana na uelewa kuhusu matatizo ya kiakili. Watu wengi wanaamini kuwa walio na matatizo ya kiakili wanapaswa kupokea matibabu na usaidizi kutoka kwa wahudumu wa afya sawa na watu wenye matatizo ya mwili. Tunaamini pia kwamba unaweza kupona magonjwa ya akili.
Jadilianeni pamoja
- Jadilianeni pamoja kuhusu mitazamo kuhusu afya ya kiakili katika vipindi tofauti na katika jamii mbalimbali.
- Je, tunaweza kufanya nini ili kuimarisha afya ya akili?
Chagua jibu sahihi
Je, watu wengi nchini Norwe wanachukulia vipi matatizo ya kiakili?
Chagua jibu sahihi
Je, ni nani anaweza kupata matatizo ya kiakili?
Chagua jibu sahihi
Je, daktari wako wa kawaida anapaswa kufanya nini ikiwa unahitaji mtu wa kuzungumza naye?
Chagua jibu sahihi
Je, matatizo ya kiakili yanaweza kutuathiri vipi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?