Nyumba
Tazama filamu
Nyumba
Nyumba
Kuna kati ya nyumba milioni 2.7 na 3 nchini Norwei. Karibu nusu ya idadi hii ni nyumba za familia moja. Katika miji mikubwa kama Oslo, nyumba nyingi ziko kwenye fleti. Katika manispaa ndogo, nyumba za familia moja zinawakilisha nyumba nyingi huko. Karibu asilimia 82 ya familia zinamiliki nyumba zao, huku asilimia 18 iliyosalia wanakodisha nyumba.
- Nyumba moja kwenye fleti: Unamiliki nyumba yako. Unaweza kuikarabati utakavyo na kuikodisha kwa yeyote. Unalipa gharama zote zinazohusiana na nyumba yako (ushuru wa manispaa, bima ya nyumba na gharama za huduma husika). Unajinunulia nyumba mwenyewe.
- Ushirika wa makazi: Una hisa katika shirika la nyumba. Una haki ya kipekee ya kuishi kwenye nyumba. Sharti uzingatie sheria na kanuni za shirika la nyumba. Unaweka amana wakati wa kununua nyumba, na unaigharamia. Pia unalipa kodi kila mwezi. Kodi hutumika kulipia dei lako kwenye shirika la nyumba, ushuru wa manispaa na bima ya nyumba.
Kulipia
Kununua nyumba hugharimu pesa nyingi, na watu wengi hukopa pesa kutoka kwenye benki. Kawaida watu hulipia mkopo kila mwezi kwa miaka mingi. Huwezi kukopa benki kiasi chote cha bei ya kununua nyumba. Unahitaji pia kuwa na pesa zako mwenyewe. Hii inajulikana kama "mtaji/fedha za kibinafsi". Kanuni kuu ni kwamba sharti uwe na akiba yako mwenyewe ambayo ni asilimia 15 ya bei ya nyumba. Unaweza kukopa benki asilimia 85 ya bei ya nyumba. Hata hivyo, sharti uwe na mapato ya kawaida au dhamana nyingine ya kifedha ili uruhusiwe kukopa pesa kutoka kwenye benki. Benki lazima iwe na uhakika kuwa wanaokopa wanaweza kulipa riba na malipo ya polepole.
Jadilianeni pamoja
- Jadili kuhusu manufaa na changamoto za kumiliki au kukodisha nyumba yako.
- Jadili kuhusu tofauti kati ya kumiliki nyumba katika fleti na nyumba katika mashirika ya nyumba (ushirika wa makazi).
- Je, maoni yako ni gani kuhusu kuchukua mkopo wa benki? Je, inahusisha nini?
- Unaweza kwenda kwenye finn.no au tovuti nyingine ili uangalie nyumba zinazouzwa katika eneo unaloishi. Je, unaona nyumba za aina gani? Zinagharimu pesa ngapi?
Chagua jibu sahihi
Je, kuna nyumba ngapi nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, unapendelea chaguo lipi la nyumba:
- kuwa na haki ya kipekee ya kutumia nyumba yako
- sharti uzingatie sheria na kanuni
- kulipa amana unaponunua nyumba kwenye fleti
- kulipa kodi kila mwezi
Chagua jibu sahihi
Je, unahitaji kuwa na asilimia ngapi ya bei ya nyumba ili uweze kuinunua? Je, unaweza kukopa benki kiasi gani?
Chagua jibu sahihi
Je, kumiliki nyumba kwenye fleti kunamaanisha nini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?