Makundi makubwa na madogo nchini Norwe
Makundi makubwa na madogo nchini Norwe
Daima watu wamehama-hama. Mfano mmoja wa hivi majuzi ni uhamiaji kutoka Ulaya kwenda Marekani. Zaidi ya Wazungu milioni 30 walihamia huko kuanzia 1820 hadi 1930. Takriban watu laki nane walihama kutoka Norway.
Watu wengi wanaoishi Norwe ni wenyeji asilia. Watu wengi wamehamia Norwe katika miaka 60 iliyopita. Wengine wamekuja kama wakimbizi na wengine wamekuja kutafuta kazi. Wametoka Ulaya na kote ulimwenguni.
Kufikia mwaka wa 2024, Norwe ina takriban watu milioni 5.5. Zaidi ya milioni moja kati yao walizaliwa nchi zingine au wazazi wao wametoka nje ya nchi. Hiyo ni takriban asilimia 20 ya idadi ya watu wanaoishi Norwe. Karibu nusu ya wahamiaji nchini Norwe ni raia humo. Makundi makubwa zaidi ya wahamiaji hutoka Polandi, Lithuania, Ukraine, Uswidi na Syria. Wahamiaji wanaishi katika manispaa zote nchini Norwe. Hata hivyo, wahamiaji wengi wanaishi mijini kuliko vijijini.
Makundi ya walio wachache nchini
Makabila kadhaa yanayoishi Norwe yana uhusiano wa zamani na nchi hii. Makundi haya yanajulikana kama wachache nchini. Makundi haya ya walio wachache nchini ni:
- Wasami
- Wayahudi
- Kven/Wanorwe wa Ufini
- Wafini Wanaoishi Msituni
- Waroma (Jipsi)
- Romani/Tater
Chanzo: regjeringen.no
Mnamo 1999, Norwe iliidhinisha mkataba kuhusu haki za walio wachache nchini. Mkataba huu unabainisha kwamba serikali kuu ina wajibu wa kuwawezesha walio wachache nchini ili kuhifadhi na kukuza itikadi zao, pamoja na dini, lugha, mila na urithi wao wa kitamaduni.
Utangamano
Lengo la kisiasa la Norwe ni kuwa jamii ambapo walio wengi na walio wachache wanaweza kuishi pamoja kwa amani na kuhisi wao ni sehemu ya nchi yetu. Lengo kuu la sera ya utangamano ni kwa wahamiaji na watoto wao pia kuweza kutumia rasilimali zao na kuchangia katika jamii sawa na makundi ya walio wengi. Mojawapo ya vigezo vya kuhakikisha hili linatendeka ni kwamba kila mtu anayeishi Norwe anafahamu vyema lugha ya Kinorwe.
Jadilianeni pamoja
- Je, kuna uhamiaji kiasi kingi kuingia au kutoka nchi yako?
- Je, kwa nini watu huhamia nchi zingine?
- Unadhani ni kwa nini wahamiaji wengi wanaishi mijini kuliko vijijini?
- Katika baadhi ya miji, kuna wilaya za miji ambapo idadi kubwa ya wakaazi ni wahamiaji. Je, unadhani hii imesababishwa na nini? Je, unadhani hili ni jambo nzuri? Je, kwa nini ni muhimu au si muhimu?
- Je, wahamiaji wanapaswa kujifunza lugha ya nchi wanayohamia? Je, kwa nini ni muhimu au si muhimu?
- Je, wahamiaji wanapaswa kuanza kuwa na mitazamo sawa na, au kuishi kama wenyeji katika nchi wanayohamia? Je, kwa nini ni muhimu au si muhimu?
- Je, kuna makundi ya walio wachache katika nchi yako?
- Jadili kuhusu wajibu wa serikali kuu katika kuchukua hatua kuhifadhi utamaduni wa walio wachache nchini.
Chagua jibu sahihi
Takriban wakaaji wangapi wa Norwe walizaliwa nchi zingine au wazazi wao wametoka nje ya nchi?
Chagua jibu sahihi
Je, wahamiaji wengi wanaishi wapi?
Kamilisha sentensi
Ili wahamiaji waweze kutumia rasilimali zao, ni muhimu kuwa na...
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?