Shule ya msingi na shule ya kati
Shule ya msingi na shule ya kati
Maelezo kuhusu shule ya msingi na ya kati nchini Norwe:
- Watoto wote nchini Norwe wana haki ya kupata elimu kwa miaka 13 . Shule ya msingi na ya kati inachukua miaka kumi.
- Grunnskole (shule ya msingi na ya kati ) ni ya lazima na hailipishwi.
Watoto huanza shule mwezi Agosti katika mwaka ambapo wanafikisha umri wa miaka sita. - Kiwango cha Grunnskole kimegawanywa katika shule ya msingi (darasa la 1-7) na shule ya kati (darasa la 8-10).
- Katika shule ya msingi, wanafunzi hutahiniwa kwa njia ya mdomo au maandishi, lakini hakuna alama zinazotolewa.
- Katika shule ya kati, wanafunzi wanapewa alama. Wanapewa alama kuanzia 1 hadi 6, 6 ndio alama ya juu zaidi.
- Katika shule ya kati, wanafunzi pia hupewa alama kulingana na unadhifu na tabia. Alama hizo tatu ni: nzuri, ya kuridhisha na duni.
- Wanafunzi wote wa shule ya msingi na ya kati husonga darasa linalofuata, baada ya kutoka likizo za majira ya kiangazi. Hakuna mwanafunzi anayerudia darasa mara mbili.
- Wanafunzi hawavai sare za shule.
- Adhabu ya viboko ni marufuku nchini Norwe, shuleni na nyumbani.
- Masomo mengine hufanyika nje ya jengo la shule. Mifano inajumuisha matembezi, kambi ya shule, kujifunza kuogelea na ziara za majumba ya makumbusho.
- Watoto wengi nchini Norwe wanaenda shule za umma, lakini takriban asilimia tano wanaenda shule za msingi za binafsi. Kisha wazazi hulipa ada ya utumiaji, asilimia maalum ya bei.
- Masomo yanayofundishwa katika shule za msingi na za kati ni Hisabati, Kinorwe, Kiingereza, Lugha za Kigeni, Masomo ya Asili, Masomo ya kijamii, Elimu ya mazoezi ya mwili, Ukristo, dini, maadili na falsafa za maisha (KRLE), Sanaa na ufundi, Muziki, Chakula na afya, na masomo mengine ya Kuchagua.
Shule za msingi na za kati zinatumia utaratibu sawa kote Norwe, na wanafunzi wote wanafundishwa mtaala sawa. Mitaala ya kitaifa huidhinishwa na wanasiasa kwenye bunge la Storting. Hii inamaanisha kwamba wanafunzi watapata elimu sawa bila kujali manispaa wanakoishi.
Sawa na shule za chekechea, taarifa ya lengo ya shule za Norwe inasema kwamba wanapaswa kukuza maadili ya kimsingi ya Kikristo na desturi za kibinadamu, kama vile kuwaheshimu watu. Pia wanazingatia uhuru wa kiakili, upendo, msamaha, usawa na mshikamano.
Wanafunzi katika shule za Norwe hufanya kazi sana katika vikundi, na mara nyingi wao hufanya miradi. Kwa hivyo watoto hujifunza kushirikiana na kuwajali wengine.
Watoto wote katika shule ya msingi na ya kati nchini Norwe wana haki sawa ya kupata elimu. Usaidizi wa ziada hutolewa kwa wanafunzi wanaohitaji. Wanafunzi hawapaswi kuchukuliwa tofauti kwa misingi ya wanakoishi, asili yao ya familia au jinsia. Shule maalum ni chache sana nchini Norwe. Watoto wengi hupata usaidizi wanaohitaji katika shule iliyo karibu na wanakoishi.
Jadilianeni pamoja
- Je, mfumo wa elimu nchini Norwe unafanana au unatofautiana vipi na mfumo wa elimu unaojua?
- Je, mtazamo wako ni upi kuhusu maadili yaliyojumuishwa kwenye taarifa ya lengo la shule?
- Jadili kuhusu kuwapa wanafunzi alama shuleni.
- Jadili kuhusu matumizi ya sare shuleni.
Chagua jibu sahihi
Je, watoto huanza shule lini?
Chagua jibu sahihi
Je, ni asilimia ngapi ya watoto wanaosoma shule za kibinafsi nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Katika shule ya kati, wanafunzi hupewa alama kulingana na unadhifu na tabia. Je, wao hupewa alama zipi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?