Afya

  • Je, nini maana ya afya nzuri?
  • Je, ni nani anayewajibikia afya ya wakaazi wa nchi yoyote ile?
  • Je, tunaweza kufanya nini kutunza afya yetu?
  • Je, kutunza afya yako inamaanisha kuwa unapaswa kuwazia mambo mengine unapoishi Norwe, tofauti na ulipokuwa katika nchi yako asilia?
  • Je, wewe huwa na matarajio gani unapokwenda kumwona daktari?
  • Je, unafikiri ni muhimu kumwona daktari hali zipi zikitokea?

Afya nzuri – sio tu kutokuwa mgonjwa?

Wapo watu wanaosema kwamba afya nzuri inamaanisha kutokuwa mgonjwa. Wengine nao husema kuwa afya nzuri inamaanisha kuwa mwenye siha na kufurahia maisha. Zote ni fafanuzi sahihi za afya nzuri. Ufafanuzi wa kwanza hutumika sana katika jamii ambapo umaskini na magonjwa hatari yameenea. Katika baadhi ya jamii, ambapo dawa za magonjwa mengi na huduma muhimu za matibabu zinapatikana kwa kila mtu, watu wengi huchukulia kwamba afya nzuri inamaanisha afya ya mwili na akili, na mengine mengi.

Je, ni nani anayewajibikia afya yetu?

Iliaminika kuwa mamlaka ya afya ndiyo inayowajibikia afya ya wagonjwa. Katika miaka ya hivi majuzi, imekuwa bayana kwamba sisi ndio tunaowajibikia zaidi afya yetu wenyewe. Jinsi tunavyoishi inaathiri afya yetu. Mamlaka za afya zinahusika katika kutoa ushauri na mwongozo, lakini ni jukumu letu kuzingatia ushauri huo. Unaweza kupata maelezo kuhusu kuzuia na kutibu magonjwa kwenye intaneti, katika ofisi ya daktari au kwenye duka la dawa.

Aygül: Mianzi ya pua imefungana na nina maumivu ya kichwa
Daktari: Naam, huenda una mafua. Una mwasho kwenye koo pia?
Aygül: La, lakini ninakohoa kidogo.
Daktari: Huenda utapata nafuu baada ya wiki moja. Hali yako isipoimarika kufikia mwishoni mwa wiki ijayo, unaweza kuweka miadi tena.
Aygül: Je, nitapewa dawa zozote?

Katika nchi nyingi, wagonjwa wamezoea daktari kuwa mtu mwenye mamlaka ambaye huamua matibabu ya mgonjwa. Huenda wagonjwa wengine wamezoea kupata dawa kabla ya kuondoka kwa daktari. Nchini Norwe, madaktari kawaida hujadili na wagonjwa wao matibabu na taratibu mbalimbali zitakazotumika.

Tips til undervisningen

Snakk sammen

Stikkord til diskusjonen: ha energi og overskudd, ikke være syk, føle velvære, fysisk kontra psykisk helse, bruk av medisiner, kroniske sykdommer, forebygging, livsstil, kosthold, trening, alkoholvaner, tobakk, informasjon, tannhelse, smittevern, økonomiens betydning for valgmulighetene, påkledning, forkjølelse

Snakk sammen om deltakernes forventninger til legebesøk, hva de er vant til fra tidligere og hva de kan forvente i Norge.

Snakk om kunstverket

Maleri. Mor ved sengen til sin syke datter.
Foto: Nasjonalmuseet/Børre Høstland «Det syke barn» malt av Edvard Munch (1885–1886).

Tips til undervisninga

Snakk saman

Stikkord til diskusjonen: ha energi og overskot, ikkje vere sjuk, kjenne velvære, fysisk kontra psykisk helse, medisinbruk, kroniske sjukdomar, førebygging, livsstil, kosthald, trening, alkoholvanar, tobakk, informasjon, tannhelse, smittevern, kva økonomi har å seie for ein person sine valmoglegheiter, påklednad, forkjøling

Snakk saman om kva deltakarane ventar seg av eit legebesøk, kva dei er vane med frå før og kva dei kan vente i Noreg.

Snakk om kunstverket

Maleri. Mor ved sengen til sin syke datter.
Foto: Nasjonalmuseet/Børre Høstland «Det syke barn» malt av Edvard Munch (1885–1886).