Vyama vya wafanyakazi
Vyama vya wafanyakazi
Wafanyakazi pamoja na waajiri nchini Norwe wana mashirika yao yanayolinda haki na fursa zao za kushirikiana kwenye makubaliano muhimu. Takriban asilimia 50 ya wafanyakazi nchini Norwe ni wanachama wa chama cha wafanyakazi/shirika la wafanyakazi.
Wajibu muhimu zaidi wa chama cha wafanyakazi ni kujadiliana na waajiri kuhusu malipo na haki zingine za wafanyakazi. Haki hizi zinaweza kuwa saa za kazi, likizo, na haki ya kupata mafunzo kazini. Mazungumzo yanapokamilika, mikataba huandikwa na kuzingatiwa na waajiri na wafanyakazi. Wahusika wakishindwa kuafikiana, wafanyakazi wana haki ya kugoma.
Waajiri na wafanyakazi sharti washirikiane katika makubaliano tofauti ili kudumisha mazingira yanayofaa kazini. Hivyo basi, hali ya ajira nchini Norwe inawezesha ushiriki wa wafanyakazi na inadumisha demokrasia kazini. Wafanyakazi binafsi wana haki ya kusikilizwa na kushiriki katika kupanga utendakazi wao. Kupitia vyama vyao vya wafanyakazi, wafanyakazi hushiriki katika mazungumzo na hupokea habari kuhusu hali ilivyo.
Waajiri wote wana jukumu la kulinda afya, usalama na mazingira (HMS) kazini. Kazi hiyo ya HMS inapaswa kupangwa na kufuatiliwa na mwakilishi wa wafanyakazi, mwakilishi wa usalama na mwakilishi wa usimamizi.
Jadilianeni pamoja
- Je, vyama vya wafanyakazi ni muhimu katika nchi yako?
- Jadili kuhusu haki ya kugoma na hali ambapo haki hii inaweza kutumiwa.
- Je, unadhani ni kwa nini watu wengi hujiunga na chama cha wafanyakazi?
- Je, unadhani ni kwa nini karibu nusu ya wafanyakazi huamua kutojiunga na chama cha wafanyakazi?
Chagua jibu sahihi
Asilimia gani ya wafanyakazi nchini Norwe ni wanachama wa chama cha wafanyakazi/shirika la wafanyakazi?
Chagua jibu sahihi
Je, wajibu muhimu zaidi wa vyama vya wafanyakazi ni upi?
Chagua jibu sahihi
Je, wafanyakazi wanaweza kuchukua hatua gani wasipoafikiana na waajiri?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?