kuchambua mambo kwa makini na kuelewa maadili
kuchambua mambo kwa makini na kuelewa maadili
Leo, kuna msisitizo nchini Norwe kuwa kila mtu aruhusiwe kutoa maoni yake. Watoto hujifunza shuleni kuwa na hamu ya kufahamu mambo na kutumia maarifa wanayopata ili kufanya maamuzi yanayofaa. Wanajifunza kuwazia mambo, kujadili na kuwa wabunifu. Haitoshi tu kurudia alichosema mwalimu au kilichoandikwa kwenye vitabu. Ili kukuza maarifa na ufahamu mpya, sharti uulize maswali na utathmini mambo yayochukuliwa kuwa ya kweli. Pia, lazima ufahamu kuwa kuna uwezekano kwamba huenda ujuzi na uzoefu wako una upungufu fulani.
Tunaishi katika jamii ambapo maelezo yanapatikana kote. Hakuna mtu anayeweza kuhifadhi habari yote akilini. Hii inamaanisha kwamba ni muhimu kujua mahali habari inakopatikana na jinsi ya kuifikia. Miongoni mwa mambo mengine, lazima tujifunze kutumia Intaneti na kutafuta habari kwenye vitabu. Mtu yeyote anaweza kuchapisha maelezo mtandaoni, na sio habari zote zinazopatikana hapo ni sahihi. Ndio maana tunapaswa kuchambua vyanzo.
Kuchambua vyanzo inamaanisha kutathmini unachosoma. Msomaji lazima ajiulize maswali muhimu, k.m.:
- Je, aliyeandika ni nani?
- Je, aliyeandika ana nia mahususi?
- Je, madhumuni yake ya kuandika makala haya ni gani?
- Je, maelezo ni sahihi?
- Je, maelezo yote muhimu yamejumuishwa, au yapo maelezo yaliyoachwa nje?
Ikiwa tutatumia maandishi ya watu wengine, picha, muziki, nk. katika matoleo yetu wenyewe, lazima kila wakati tueleze ni nani ana hakimiliki ya vipengee hivyo.
Uelewa wa maadili unahusu kuangalia vigezo mbalimbali, ili uone chaguo zako na ufanye uamuzi bora. Hii itakuwezesha kufanya kile kinachofaa kwa jamii, watu walio karibu nawe na kwako mwenyewe.
- Uelewa wa maadili, unaomaanisha kuangalia vigezo mbalimbali, ni muhimu katika kukuwezesha kuwa mtu wa kuwazia mambo na mwenye kuwajibika. Masomo na mafunzo sharti yakuze uwezo wa wanafunzi wa kufanya tathmini za kimaadili na kumsaidia kutambua masuala ya maadili.
- Kuchambua mambo kwa makini na kuelewa maadili kunahitajika na ni sehemu ya kile kinachochukuliwa kuwa kujifunza katika hali anuwai na hivyo itawasaidia wanafunzi kuweza kufanya maamuzi yanayofaa.
Chanzo: Idara ya Elimu
Jadilianeni pamoja
- Je, kuchambua chanzo ni nini?
- Je, kuna umuhimu gani kwa wanafunzi na watu wengine kuuliza maswali kuhusu wanachosoma mtandaoni?
- Shule nchini Norwe zinahimiza wanafunzi kufikiria na kuwa na mitazamo yao binafsi. Je, unachukulia hili vipi? Je, kwa nini iko hivyo? Je, inaathiri malezi ya watoto na uhusiano kati ya watoto na wazazi wao?
Familia ya watu wanne inahitaji gari mpya. Gari litatumika kwa safari ndefu na fupi. Martin na Maria hawajui cha kuchagua.
1. Gari kubwa lenye viti sita wanaloweza kutumia kwa safari ndefu na fupi. Gari lina nafasi ya kubebea nyanya na babu, na linatumia dizeli.
2. Gari la umeme lenye viti vinne linalofaa kwa safari fupi za familia, lakini linahitaji chaji njiani wakati wa safari ndefu za familia, na halina nafasi ya kubebea babu na nyanya.
Martin na Maria hawangependa kuathiri mazingira, na wao ndio jamaa wa karibu wa babu na nyanya. Je, unadhani Martin na Maria watajadili masuala yepi ya kimaadili?
Chagua jibu sahihi
Je, kuchambua chanzo ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, ni hali ipi itafaa nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, unapaswa kuchunguza nini unaposoma kitu fulani kwenye mtandao? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?