Ushirikiano kati ya shule na wazazi au walezi
Ushirikiano kati ya shule na wazazi au walezi
Binti: Hii hapa barua kutoka kwa mwalimu wangu. Tunahitajika kwenda kwenye mazungumzo ya ukuzaji wa wanafunzi wiki ijayo.
Nyanya: Kwa nini mwalimu ameandika barua? Umekosea?
Binti: La, ni mkutano wa kawaida tu na mwalimu. Kila mwanafunzi amepewa barua.
Nyanya: Una uhakika hujafanya chochote kibaya? Nilipokuwa mwanafunzi, wazazi walizungumza tu na mwalimu wakati watoto wao walikuwa wamefanya makosa.
Mama: Kwa kweli, sio hivyo tena. Ningependa kuzungumza na mwalimu ili kujua mambo yalivyo. Pia nina maswali machache kuhusu kazi ya shule ya kufanyia nyumbani.
Wazazi wana jukumu kuu la kuwajibikia watoto wao. Hata hivyo, watoto na vijana watasaidika wazazi wao wakishirikiana na chekechea na shule katika kukuza malezi na elimu yao.
Wazazi, shule, pamoja na mwanafunzi, sharti wahakikishe kuwa mtoto anajifunza kile anachohitaji. Mwanafunzi, wazazi na mwalimu sharti wajadiliane kuhusu kukuza mwanafunzi kimasomo na jinsi mwanafunzi anavyoendelea shuleni, angalau mara mbili kwa mwaka.
Ni muhimu kwa wazazi kusoma na kufahamu yote wanayoandikiwa kutoka shuleni. Wazazi wanaweza kuwasiliana na mwalimu au wafanyakazi wengine wa shule ikiwa wana maswali.
Jadilianeni pamoja
- Inamaanisha nini tunaposema kwamba shule inapaswa kuwa mahali pazuri kwa watu wote?
- Je, "kushiriki katika maamuzi" na "jukumu la pamoja" haswa zinamaanisha nini?
Wakati mwingine ushirikiano haufanyi kazi jinsi tunavyotaka. Wazazi na shule wanaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu kile ambacho ni muhimu na sahihi. Tatizo lingine linaweza kuwa ni kwamba shule na wazazi wana matarajio tofauti kwa kila mmoja. Walimu wengine wanaweza kueleza kuhusu hali hizi:
- Wazazi hawahudhurii mikutano ya wazazi au vikao vya ukuzaji wa wanafunzi.
- Wakati wa likizo ya majira ya joto, wazazi huwapeleka watoto wao nchi walikotoka kisha hawarudi shule zinapofunguliwa mwezi Agosti. Watoto hurejea shuleni wiki au miezi michache baadaye.
- Watoto waliozaliwa nchini Norwe wana ujuzi duni wa lugha ya Kinorwe wanapoanza shule.
- Wazazi hawataki wanafunzi wao kushiriki katika shughuli za masomo nje ya shule, k.m. kambi za shule.
- Wanafunzi hawaruhusiwi kushiriki katika mazoezi ya mwili au kufunzwa kuogelea.
- Kwa nini wazazi wengine huamua hivi?
- Je, watoto wanaweza kuathirika vipi?
- Jadili hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kutatua matatizo haya.
Chagua jibu sahihi
Je, walimu, wanafunzi na wazazi hujadiliana mara ngapi kuhusu kukuza mwanafunzi kimasomo na jinsi mwanafunzi anavyoendelea shuleni?
Chagua jibu sahihi
Je, mtu hujadili yepi katika mazungumzo na mwalimu?
Chagua jibu sahihi
Wakati mwingine ushirikiano haufanyi kazi kama tunavyotarajia. Tatizo linaweza kuwa nini? Unaweza kuchagua zaidi ya jibu moja.
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?