Maendeleo endelevu
Tazama filamu
Maendeleo endelevu
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ni mpango wa pamoja wa maendeleo endelevu, kote ulimwenguni. Lengo la malengo haya ni kumaliza umaskini, kukabiliana na aina tofauti za ukosefu wa usawa na kukomesha mabadiliko ya hali ya hewa ifikapo 2030.
Mabadiliko ya tabianchi
Hali ya hewa na tabianchi ni mambo mawili tofauti. Hali ya hewa ndiyo unayoona kila siku ukiwa nje au unapotazama kwenye dirisha, nayo tabianchi ni wastani wa hali ya hewa kwa muda mrefu. Katika miaka 100 iliyopita, mabadiliko makubwa yametokea katika hali ya hewa duniani. Watafiti wengi wa hali ya hewa ulimwenguni wanaamini kwamba uzalishaji wa kaboni unaotekelezwa na binadamu ndio umesababisha mabadiliko ya haraka na yenye madhara makubwa tunayoona leo.
Mabadiliko tunayoona ni pamoja na:
- Kiwango cha joto kinaongezeka duniani.
- Maji yanaongezeka baharini na yanazidi kuwa yenye asidi.
- Barafu inayeyuka.
- Kiwango cha mvua kimebadilika sana na hali ya hewa imekuwa mbaya zaidi.
Rasilimali zinazozalishwa upya
Rasilimali zinazozalishwa upya ni kauli inayorejelea maliasili zinazoweza kujitengeneza. Watu wanaweza kutumia rasilimali hizi, na zikitumiwa ipasavyo, haziwezi kukwisha.
Mifano ya rasilimali zinazozalishwa upya:
- wanyama, miti na mimea
- mvua, upepo na maji
- mwanga wa jua
Mifano ya rasilimali zisizozalishwa upya:
- mafuta
- gesi
- makaa
Chakula kinachozalishwa nchini
Chakula kinachozalishwa nchini kinakuzwa karibu na wanakoishi walaji. Chakula kinapozalishwa nchini, hakihitajiki kusafirishwa hivyo inapunguza uchafuzi wa hewa kutokana na usafirishaji. Pia ni rahisi kudhibiti uzalishaji wa chakula kinachozalishwa nchini. Hii inaweza kuhusisha viua-wadudu vinavyonyunyizwa, matumizi ya viua-viini kwa nyama na samaki na maslahi ya wanyama.
Jadilianeni pamoja
- Jadili kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Je, inaathiri vipi nchi yako? Je, inaathiri vipi nchi ya Norwe?
- Jadili kuhusu rasilimali zinazozalishwa upya. Je, kipi hutokea watu wanapotumia rasilimali hizi kwa haraka zaidi kuliko kiwango cha uzalishaji wake?
- Jadili kuhusu manufaa na changamoto za vyakula vinavyozalishwa nchini.
- Je, ni muhimu kwa nchi kujitegemea? Kwa nini ni muhimu au si muhimu?
- Jadili kuhusu malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu. Je, unadhani baadhi ya malengo hayo ni muhimu zaidi kuliko mengine? Je, mataifa yote yanazingatia malengo haya?
Chagua jibu sahihi
Je, tabianchi ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, kulingana na watafiti wengi wa hali ya hewa, mabadiliko makubwa na ya haraka katika hali ya hewa yamesababishwa na nini?
Chagua jibu sahihi
Rasilimali zinazozalishwa upya ni nini?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?
Bofya picha sahihi
Je, ni picha ipi inayoonyesha rasilimali isiyozalishwa upya?