Mahali pa kutangamana
Mahali pa kutangamana
Mahali pa kutangamana ni sehemu ambapo watu hukutana. Watu hutangamana kupitia njia mbalimbali. Familia, ya karibu na jamaa, zinaweza kuwaleta watu pamoja. Shuleni na kazini ni sehemu muhimu ambapo watu wengi hutangamana. Watu wengi hukutana na marafiki zao wakati hawana shughuli. Wanaweza kukutana kwenye mkahawa au manyumbani kwao. Watu wazima wengi huendeleza masomo yao au hufanya kozi mbalimbali wakati hawana shughuli. Watu wengine huimba kwenye kwaya au hucheza ala, na wengine wanahusika katika mashirika mbalimbali. Hizi pia ni sehemu za watu kutangamana.
Shughuli za burudani zilizopangwa
Watoto wengi hushiriki katika shughuli mbalimbali za burudani. Wanaweza kujiunga na bendi ya muziki au timu ya michezo. Wengine ni Wanaskauti, na wengine hujiunga na kikundi cha kupiga picha. Wazazi wanahusika katika shughuli hizi. Huenda ukapata mamake mtoto fulani ni mkufunzi wa timu ya wasichana ya mpira wa mikono. Wazazi wanaweza kubadilisha zamu katika kuwapeleka na kuwachukua watoto katika shughuli mbalimbali. Hii inaweza kuwa njia nzuri ya kufahamiana na wakaazi wa eneo kwa watu ambao wamefika Norwe hivi majuzi au wamehamia eneo jipya.
Kazi ya hiari
Kazi ya hiari ni kazi ambayo ni tofauti na ajira ya kawaida. Hakuna kulipwa mshahara. Kazi ya hiari ni ya muda mfupi - hakuna mtu anayefanya kazi wakati wote kwa hiari! Kazi ya hiari mara nyingi huhusishwa na mashirika yanayohudumia jamii. Mfano unajumuisha Shirika la Msalaba Mwekundu, vilabu vya michezo, hafla za kitamaduni nk.
Watu wengi hushiriki katika mashirika ya hiari katika nchi za Scandinavia. Mashirika haya hutoa fursa ya kujifunza vitu vipya na kupata marafiki wapya. Mengi ya mashirika haya pia huwasaidia watu kufahamu kuhusu demokrasia. Wanaohusika hujifunza kuhusu vigezo vya demokrasia kama vile kushiriki katika mikutano, uchaguzi na kura. Mashirika mengi ya hiari pia huchangia katika michakato ya kisiasa ya eneo na kitaifa.
Kuhusika katika shirika moja au zaidi la hiari hukuwezesha kufahamiana na watu mahali unapoishi na inakuwezesha kuhisi wewe ni sehemu ya jamii. Utafahamiana na watu zaidi, na hili linaweza kuleta mabadiliko katika kazi, elimu na maisha ya kila siku.
Kuwa pamoja
Kuna sheria na kanuni nyingi rasmi katika jamii zote. Pia kuna sheria nyingi ambazo kila mtu anajua, lakini hazijaandikwa. Sheria hizi ni tofauti katika jamii mbalimbali. Mfano mmoja ni jinsi tunavyosalimiana. Nchini Norwe, ni kawaida kwa wanaume na wanawake kusalimiana kwa mikono. Ni kawaida pia kusalimiana kwa mikono mnapoagana. Marafiki husalimiana kwa kusema ‘hujambo’, kukumbatiana au kugusana bega. Kawaida watu husalimiana: ‘Hujambo, unaendeleaje?’ Jibu la kawaida ni: ‘Niko salama, nashukuru. Wewe je?'
Mhamiaji: Je, ungependa kunitembelea siku moja?
Mnorwe Ndiyo, ningependa sana.
Mwezi mmoja baadaye:
Mhamiaji: Kwanini hukunitembelea?
Mnorwe Hujanialika.
Nini kilitokea? Nchini Norwe unapaswa kumwalika mtu siku na saa mahususi. Wanorwe huwa hawatembelei marafiki bila kupanga mapema.
Jadilianeni pamoja
- Je, ni muhimu kwa wazazi kuwahimiza watoto wao kushiriki katika shughuli maalum za burudani? Je, kwa nini ni muhimu au si muhimu?
- Je, unajua ikiwa kuna mashirika yoyote ya hiari mahali unakoishi?
- Jadili kauli ‘Bila kuwepo kwa wanaojitolea, shughuli zitasimama nchini Norwe’.
- Je, kuna manufaa gani ya kufanya kazi ya hiari?
- Toa mifano ya sheria zisizo rasmi ambazo ulikuwa unajua.
- Toa mifano ya sheria zisizo rasmi nchini Norwe.
- Kuna tofauti kubwa katika jinsi jamii mbalimbali zinavyochukulia wageni, watu kulala kwao, kile mwenyeji anahitajika kufanya, muda wa kutembeleana nk. Jadili tofauti hizi.
Chagua jibu sahihi
Je, nini maana ya mahali pa kutangamana?
Chagua jibu sahihi
Je, kazi ya hiari ni nini?
Chagua jibu sahihi
Je, kawaida unamsalimia mtu vipi unapokutana naye kwa mara ya kwanza nchini Norwe?
Chagua jibu sahihi
Je, kuna manufaa gani ya kufanya kazi ya hiari?
Chagua taarifa sahihi au isiyo sahihi
Soma taarifa hizi. Ipi ni sahihi? Ipi si sahihi?